WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWA MABALOZI KUBADILI MIFUMO HASI INAYOKANDAMIZA WANAWAKE KWENYE UONGOZI




Afisa Programu - Sera na Ujenzi wa Vuguvugu wa TGNP Mtandao,Shakila Mayumana akifunga warsha ya Waandishi wa habari ngazi ya jamii iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kuripoti masuala ya kijinsia ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi. Picha na Kadama Malunde 1 blog
 
Na Shushu Joel - Dar es salaam
Waandishi wa habari wametakiwa kuwa mabalozi katika kuandika habari za kubadili mitazamo hasi ya jamii juu ya wanawake kutokuwa viongozi katika jamii.



Hayo yamesemwa leo Jumatano Septemba 18,2019 na Afisa Programu - Sera na Ujenzi wa Vuguvugu TGNP Mtandao,Shakila Mayumana wakati wa akifunga warsha ya Waandishi wa habari ngazi ya jamii kutoka mikoa ya Shinyanga,Tabora,Simiyu,Mara na Kigoma yaliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kuripoti masuala ya kijinsia ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi.



Mayumana amesema endapo wanahabari wakitumia kalama zao wataisaidia jamii kuondokana na mila hasi katika jamii zinazomnyima fursa mwanamke kugombea nafasi za uongozi wa kisiasa.

"Waandishi wa habari ni watu wanaokubalika na kuthaminika katika jamii hivyo tunawaombeni mtumie fursa hii ya elimu mliyoipata hapa ili mkaisaidie jamii zetu ziondokane na mifumo hasi inayomgandamiza mwanamke",amesema.



"Naomba washiriki wa warsha hiii muende kufanyia kazi yale yote mliyojifunza katika kuhamasisha wanawake na vijana kushiriki katika uchaguzi. Fanyeni kazi zitakazotengeneza historia na kumbukumbu katika maeneo na jamii mnayoishi",ameongeza Mayumana.



Warsha hiyo ya siku tatu imefanyika Septemba 16,2019 hadi Septemba 18,2019 katika ukumbi wa TGNP Mtandao Jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa wanawake na uongozi unaotekelezwa na TGNP Mtandao na UN Women.



Lengo kuu la warsha hiyo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari juu ya kutoa taarifa zenye mrengo wa kijinsia hasa zenye kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo kubadili mitazamo na mila hasi zinazozuia ushiriki wa wanawake katika uongozi.

 Afisa Programu - Sera na Ujenzi wa Vuguvugu wa TGNP Mtandao,Shakila Mayumana akifunga warsha ya Waandishi wa habari ngazi ya jamii iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kuripoti masuala ya kijinsia ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi. Picha zote na Kadama Malunde 1 blog

Afisa Programu - Sera na Ujenzi wa Vuguvugu wa TGNP Mtandao,Shakila Mayumana akiwahamasisha Waandishi wa habari kuwa mabalozi katika kuandika habari za kubadili mitazamo hasi ya jamii juu ya wanawake kutokuwa viongozi katika jamii.

Afisa Programu  Mwandamizi TGNP Mtandao,Deogratius Temba akizungumza wakati wa kufunga warsha ya Waandishi wa habari ngazi ya jamii iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kuripoti masuala ya kijinsia ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi. 

Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo akielezea namna UTPC inavyozingatia usawa wa kijinsia katika masuala ya uongozi.
Mkufunzi wa Masuala ya Jinsia na Uongozi (Mwezeshaji) Andulile Mwabulambo akizungumza wakati wa kufunga warsha ya Waandishi wa habari ngazi ya jamii iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kuripoti masuala ya kijinsia ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi. 


Afisa Habari TGNP Mtandao,Monica John akizungumza wakati wa kufunga warsha ya Waandishi wa habari ngazi ya jamii iliyolenga kuwajengea uwezo kuhusu namna ya kuripoti masuala ya kijinsia ikiwemo kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye nafasi za uongozi.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post