Kipindi cha radio kilichowarudisha nyumbani watoto walionusurika mauaji ya kimbari Rwanda

Maelfu ya watoto walikua miongoni mwa wakimbizi waliotoroka Rwanda baada ya mauaji ya kimbari

Hii ni simulizi ya wavulana wadogo watatu ambao walikaribia kuangamia katika wimbi la watu waliokua wakitoroka ghasia na mauaji yaliokumba Rwanda mwaka 1994.

Pia ni inaangazia jinsi matangazo ya radio yalivyochangia kuwaokoa na kuwarejesha nyumbani watoto waliotenganishwa na familia zaa kwa zaidi ya mwongo mmoja.

"iliturudishia matumaini," Theogene Koreger aliimbia BBC, miaka 25 baada ya mpwa wake kutoweka.

"Ujumbe ulifika sehemu ambazo hatukuweza kufika - waliwasilisha ujumbe ambao bila shaka haungetufikia."

Makala hya yanaanzia mwisho wa mauaji wa kimbari ya Rwanda. Siku mia moja ya mauaji na ubakaji iliosababisha kuawa kwa Watutsi na baadhi ya Wahutu wanaokadiriwa kuwa 800,000.

Maelfu ya wenginne walilazimika kutoroka makwao kwa kuhofia usalama wao miongoni mwao watoto wanaokadiriwa kuwa 120,000 anbaowlitenganishwa na familia zao.

Mugabo na ndugu yake mdogo wa kiume Tuyishimire walikua miongoni mwa watoto 40,000 waliovuka mpaka kutafuta mahali salama. Mugabo - ambaye alikua na miaka saba pekee- alilazimika kuwa kiongozi wa nyumba chache zilizosalia.
Mugabo (kushoto) na Tuyishimire, walipigwa picha na Red Cross walipokuwa DR Congo

Jukumu la mwisho aliloachiwa na mama yake kabla afariki, lilikua la kumtunza Tuyishimire, ambaye alikua mtoto mdogo wakati huo. Haki miliki ya picha Red Cross Image caption Mugabo (kushoto) na Tuyishimire, walipigwa picha na Red Cross walipokuwa DR Congo

Lakini hawakua peke yao katika taifa hilo ambalo sasa linafahamika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na walifanya kila juhudi kuishi katika kambi za wakimbizi zilizoibuka katika mipaka ya Rwanda.

"Tuliishi kwa kuomba omba, tomato na samaki," anakumbuka matukio hayo kwa masikitiko lakini anamshukuru Mungu kwa kumnusuru- na kusimulia masaibu hayo miaka 25 baadae.

Lakini kambi hizo zilikua mahali hatari: wakimbizi karibu milioni moja walinusurika mauaji ya kimbari walikabiliwa na na magonjwa ya kuhara na kutapika kutokana na kuishi katika mazingira machafu.

Kabla wafanikiwe kurudi nyumbani maelfu ya wengine walifariki kutokana na magonjwa hayo.

"Kambi hizo zilikua mbaya sana. Kulikua na magonjwa kila mahali," Rene Mukuruwabu aliiambia BBC akiwa ameketi katika bustani mjini Kigali maili kadhaa kutoka mahali ambako yeye na familia yake walilazimika kwenda walipolazimika kukimbilia usalama wao.

Rene, kwa njia moja, alikua miongoni mwa watu waliokua na bahati: familia yake haikusambaratika ilipofika Tanzania mwaka 1994.

Lakini baba yake alitoweka na mamayake ambaye aliweka kliniki ya kuwasaidia wagonjwa, alifariki kutokana na maambukizi ya magonjwa katika kambi ya wakimbizi.

Kufumba macho na kufungua familia yake ilisalia na yeye, ndugu yake mdogo Fabrice, na dada yake wa kambo.

Na ilichukua muda kidogo kabla ya Rene mwenye umri wa miaka mitano kujipata peke yake duniani. Image caption Rene alipoteza familia yake katika kambi ya wakimbizi ya Tanzania mwaka 1994
Rene Mukuruwabu
Rene alipoteza familia yake katika kambi ya wakimbizi ya Tanzania mwaka 1994

Baada ya mauaji ya kimbari kumalizika mwezi Julai mwaka 1994, mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yalikabiliwa na a changamoto nyingi - jinsi ya kuponya makovu ya walioumia kimawazo, jinsi ya kuwapa chakula walio na njaa, jinsi ya kuwapatia majkaazi watu walioachwa bila makao...

Na jinsi ya kuwakutanisha tena watoto waliopotea na familia zao.

Lakini - unawezaje kutekeleza wajibu huo wakati hapakua na huduma ya interneti wala simu za rununu, huku watu wakikimbia bila kubeba chochote, wakati taifa linaumbwa na machafuko na vurugu- utaanzia wapi kutafuta kilichoachwa nyuma na familia?

"Lilikua wazo la Neville Harms, ambaye alikua msimamizi wa BBC Idhaa ya Kiswahili mwaka 1994," Ally Yusuf Mugenzi anaelezea. "Aliamua kuanzisha mradi wa kuzikutanisha familia zilizotengana."

Kutokana na wazo hilo iliamuliwa hatua ya kuanzisha kipindi cha dakika ambacho kitakua kikipeperushwa hewani na BBC kikiwalenga wasikilizaji wa Rwanda na mataifa yalio karibu.

Kipindi hicho kilianza kwa Taarifa ya Habari na kufuatiwa na sauti za watu wanaowatafuta jamaa zao.

Ukweli ni kwamba haikua rahisi kutayarisha kipindi hicho lakini kwa ushirikiano na mashirika yasiokua ya kiserikali kama vile Shirika la Msalaba Mwekundu, Save the Children na Umoja wa Mataifa sauti zilizorekodiwa kutoka kwa wahasiriwa ziliwasilishwa katika studio za BBC.

"Tulipeperusha hewani sauti za watu kutoka kambi hizo za wakimbizi ," anaeleza Mugenzi, ambaye pia alikua mmoja wa watangazaji wa kipindi hicho kilichokua kikiendeshwa na watangazaji wawili.

Hatimaye tulipewa jina la Gahuzamiryango, likimaanisha "muunganishi wa familia" na mara ya kwanza ilitangazwa kwa mara ya kwanza miaka 25 iliyopita.

Kipindi hicho kilitarajiwa kumalizika baada ya miezi mitatu. Lakini muda huo ulifikia kikumo na kuendelea mbele.

Maelezo zaidi kuhusiana na mauaji ya kimbari:

Mara ya mwisho Rene alikutana na familia yake walikua wanarejea nyumbani Rwanda. Na wakati huo walikua wametoweka.

"Unaweza kutafakari hali ya mtoto aliyepotea?" aliuliza. "Nilikua nalia tu, nilipoteza matumaini. Niliona watu wengi lakini sikuona mtu yeyote wa familia yangu."

Kufikia wakati alipatikana na wafanyikazi wa kutoa misaada alikua amepoteza uwezo wa kuzungumza.

"Waliniuliza jina langu na mahali nilikotoka lakini kutokana na uoga na mfadhaiko nadhani nilishindwa kujieleza."

Hakuweza kuzungumza tena kwa miezi kadhaa, alihamishiwa makaazi ya watoto mayatima waliokabiliwa na hali kama yake, na ambao wamejipata peke yao duniani.

Lakini - baada ya kupata utulivu kutokana na familia yake mpya iliyomchukua na kumlea- sauti yake iliwafikia wengi kupitia matangzo ya redio.

"Majirani zangu walinifikia baada ya kusikia jina langu redioni," anakumbuka. Alienda nyumbani kwa majirani zao kujisikilizia mwenyewe matangazo hayo.

"Sikuweza kukumbuka jina langu, lakini nilikumbuka jina na ndungu yangu mdogo," Mugabo alifichua hayo, huku akionesha BBC picha ya wavulana wawili ambao Red Cross iligundua wanaishi peke yao nchini DR Congo.

Lakini hiyo haikutosha: nyumbani Kigali, mjomba wao Theogene pia alisikia matangazo ya redio.

"Niliposikia matangazo hayo redioni nilihisi kama nimepata ujumbe kutoka mbinguni ," alisema, kumbukumbu hiyo inamfanya atabasamu karibu robo ya krane baadae.

"Hiyo ni kwa sababu watu waliokua hapa Rwanda hawakua na njia yoyote ya mawasiliano na hatukupata ujumbe kutoka popote." Image caption Mugabo na Tuyishimire awali walikuwa waliogopa kurudi nyumbani
Ndugu wawili
Mugabo na Tuyishimire awali walikuwa waliogopa kurudi nyumbani

Hatua ya kusikia majina ilikuwa sehemu ya kuwarejesha nyumbani watoto hao. Nchi ilikuwa bado inakabiliwa na ghasia na barabara zilikuwa hatari.

Lakini hofu kubwa ya vijana hao ilikua uoga wa kurudi nyumbano.

"Niliona barua ya mjomba wangu aliyekuwa Rwanda na aliyetaka kutuona. Lakini nilikataa," Mugabo anasema.

"Nilishuhudia baba yangu akifariki, Nilimuona mama yangu akifariki, kwa nini nirudi huko?"

Halafu suala lingine: nikuwa mjomba wake alikua askari wa Rwandan Patriotic Front - wanajeshi waasi wa wa Kitutsi waliochukua uongozi wa Rwanda, na kumaliza mauaji ya kimbari.

Mugabo alikuwa akifundishwa kwamba wanajeshi hao, ni mende waliokua na mkia.

Lakini mjomba wake alikua na nafasi moja ya kujieleza: alituma picha yake akiwa na ndugu yao mwingine. Picha hiyo iliwashawishi: baada ya kuishi msituni kwa mwaka mmoja, Mugabo na Tuyishimire hatimae walikubali kwenda nyumbani.

Rene haelewi kwa nini hakufanya lolote aliposikia jina lake redioni miakayote iliopita. Pengine, ni uoga: alifahamu fika maisha yake yalikua mazuri na familia yake mpya. Ambayo ahuenda ilikua mahali salama.

Hata hivyo, alikua na matumaini huenda kuna mtu wa familia yake aliyekua anamtafuta.

"Wazo hilo lilikuwa akilini mwangu," alisema. "Nitaka tena kusikia jina langu redioni lakini hilo halikufanyika."

Hatua iliyomfanya kusalia na jina lake licha ya mama yake mlezi kupendekeza abadilishe jina kwa sababu ni mmoja wa familia hio.

Na baada ya kujiunga na mtandao wa kijamii wa Faceboo zaidi ya miaka 15 iliyopita anatafakari ikia kuna mtu atamtambua, na haikuchukua muda mrefu alipata jibu.

"Niliweka jina langu mtandaoni siku ya Jumamosi na ilipofika Jumapili,walinipata ."

"Mwaka 1995 tulijaribu kumtafuta," mjomba wa Rene, Charles aliiambia BBC. "Hatukumpata, lakini hatukumsahau. Tulidhani amefariki. Tulimweka katika kumbukumbu ya kihistoria.

"Na miaka 18 baadae, ni kama miujiza kwetu kubaini kuwa yungali hai."

Ni ndugu yake Rene, Olivier ambaye alimpata kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook - Ni yeye aliyeifahamisha familia yake kuwa kijana wao aliyetowekaamepatikana.

"Unafanana na ndugu yake mdogor," Olivier alimwambia Rene mara ya kwanza walipokutana. "Ni wewe sina shaka na hilo."

Hii ilikua mara kwanza tangu wawili hao walipotenganishwa miaka yote hiyo amabyo Rene aligundua ndugu yake aliponea. 
 
Manduga
Rene na ndugu yake mdogo Fabrice, ambaye aliletwa nyumbani na dada yake wa kambo, walikutanishwa mwaka 2012
 Matangazo ya Redio sio njia pekee iliyotumiwa na Shirika la Msalaba Mwekundu na mashirika mengine ya kutoa misaada ya kibinadamu kuwaunganisha watoto waliopotea na familia zao. 

Picha na majina ya watoto zilisambazwa kutoka kijiji kimoja hadi kingine ili kutafuta jamaa zao.

Mwisho wa mpango huo, Espèrance Hitimana, ambaye sasa ni msimamizi wa kulinda data katika Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu mjini Kigali, anakadiria walifanikiwa kuwaunganisha watu 70,000 . Lakini dhughuli hiyo bado inaendelea.

"Bado tunapoke visa kama mbili au tatu kwa mwezi,"anasema. "Visa vingine tunafanikiwa kupata familia. Katika visa ambavyo hatuna taarifa yoyote hatuna budi kuwaeleza hatuna la ziada."

Katika Idhaa ya BBC ya Maziwa makuu, japo makala ya kuunganisha familia zilizotengana - yalisitishwa.

Siku hizi inajivunia kipindi cha mjadala ambayo imeelekeza darubini yake katika mawasiliano ua kidigitali.

Mugenzi - ambaye anaongoza Idhaa ya BBC Great Lakes Service iliyobuniwa baadae - anaelezea kwa furaha isiyokua na kifani kile walichofikia katika kipindi cha miaka 25 iliopita.
Familia
Theogene anayashukuru Mashirika ya Msalaba Mwekundu na BBC kwa juhudi za kuwaunganisha familia zilizosambaratishwa na mauaji ya kimbari Rwanda

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post