Mahakama kuamua dhamana ya Mwanahabari Sebastian Atilio kesho, Kesi ya Marato yaahirishwa hadi Oktoba 22


Na Francis Godwin, Iringa

Mwandishi wa habari Sebastian Atilio anayekabiliwa kwa makosa mawili yaani kutoa taarifa ya uongo na kufanya kazi ya uandishi bila kuthibitishwa na bodi.

Jana ilikua ni siku ya kusikiliza mapingamizi yaliyowekwa na wakili wa THDC Emmanuel Chengula anaemtetea mwandishi huyo, mapingamizi hayo ni dhidi ya maombi yaliyopelekwa na jamhuri kumzuia mwandishi huyo kutopewa dhamana kwa hofu ya usalama wake dhidi ya RAIA wa kijiji cha ifupira.

Pamoja na hayo mahakama ya wilaya ya Mufindi mbele ya Hakimu Mkazi Edward Uforo ilisikiliza mapingamizi yote manne na kuahirisha kesi hiyo mpaka tarehe 25/09/2019 ambapo itatoa maamuzi juu ya hatima ya dhamana ya mwandishi Huyo wa habari.

Hata hivyo kesi yake ya msingi itatajwa tarehe 25/09/2019 Mara baada ya kusomwa kwa uamuzi unaotokana na mapingamizi yaliyo wekwa.

Mwandishi Sebastian Atilio akiingia ndani ya Mahakama ya Wilaya ya Mufindi

Wakati huo huo kesi inayomkabili Mwandishi wa habari George Marato imepangwa kusikilizwa tena  Oktoba 22 na 23 kwa upande wa mashitaka kutakiwa  kuleta ushahidi wao.

Katika shauri hilo wakili wa mshitakiwa Thomas Makongo aliwasilisha hoja kwa kutaka Mahakama itoe amri kwa TAKUKURU  kufuta taarifa yao kwa Umma waliosambaza wakiandika maneno yenye kuingilia uhuru wa mahakama na kumuhukumu mteja wake tofauti kilichopo mahakamani.

Hakimu Ndira wa mahakama ya Musoma amemtaka wakili awasilishe hoja hiyo kwa kutaja kifungu cha sheria ili Mahakama iweze kuchukua hatua.

wakili ameiomba mahakama kuwasilisha hoja hiyo na kifungu cha sheria Oktoba  22 wakati kesi hiyo itakaposikilizwa tena.

2 Comments

This is received, thanks for your comments, will come back to you

  1. nawasalimu sana.
    nimepata dhamana tarehe 27/10 na kesi ilipangwa kusikilizwa jana tarehe 10/10 hivyo iliarishwa mpaka 11/11/2019 kwa kile kinacho daiwa kuwa upelelezi haujakamilika. asanteni kwa mchango wenu wa hali na mali. kesi hii ina mlengo wa kisiasa tuu wala hoja siyo habari niliyo ichapisha.

    ReplyDelete
  2. nawasalimu sana.
    nimepata dhamana tarehe 27/10 na kesi ilipangwa kusikilizwa jana tarehe 10/10 hivyo iliarishwa mpaka 11/11/2019 kwa kile kinacho daiwa kuwa upelelezi haujakamilika. asanteni kwa mchango wenu wa hali na mali. kesi hii ina mlengo wa kisiasa tuu wala hoja siyo habari niliyo ichapisha.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post