Na Mwandishi Wetu, Arusha
Waandishi wa habari wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kuripoti taarifa mbalimbali za mahakama za kimataifa ili kuuhabarisha umma kuhusu matukio yanayoendelea katika mahakama hizo.
![]() |
Washiriki wa mafunzo kuhusu uhuru wa habari wakiwa katika majadiliano ya vikundi |
![]() |
Mshauri wa sheria wa shirika la ICNL Aloyce Habimana akiwasilisha mada kuhusu sheria zinazosimamia uhuru wa habari katika mafunzo yanayoendelea jijini Arusha kwa wanahabari |
Amesema waafrika wanapaswa kujua mambo mbalimbali ambayo yamekuwa yakiendelea katika mahakama hizo hivyo ni jukumu la waandishi wa habari kutembelea katika mahakama na kuripoti kile kinachoendelea.
Chatbar ambae ameyazungumza hayo katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la International Center for Not for Profit Law ( ICNL) lenye makao yake makuu nchini Marekani, kwa waandishi wa habari katika jiji la Arusha amesema AfCPHR imekuwa ikiwakaribisha waandishi kila mara kuripoti taarifa za mahakama hiyo na wamekuwa wakifanya vizuri.
Amesema taarifa za waandishi zimekuwa zikitoa mchango mkubwa kwa jamii za mataifa mbalimbali Afrika ambao wamekuwa wakifikisha mashauri yao katika mahakama hiyo baada ya kutoridhishwa na mahakama katika nchi zao.