Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Rais Mstaafu wa
Zambia Mhe. Keneth Kaunda na Rais Mstaafu wa Nigeria Mhe. Olubagan
Obasanjo wakiteremka kwenye Jukwaa baada ya kutowa Heshima za Mwisho
mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa la
Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Gabriel Mugabe katika Uwanja wa Taifa wa
Michezo jijini Harare Zimbabwe. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt.
John Pombe Magufuli kwenye Hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais
Kenya Mhe. Uhuru Kenyata walipokutana wakati wa Hafla ya kutowa Heshima
za Mwisho mbele ya Jeneza lenye Mwili wa Rais wa Zamani na Muasisi wa
Taifa la Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Gabriel Mugabe katika Uwanja wa
Taifa wa Michezo jijini Harare Zimbabwe. Makamu wa Rais amemuwakilisha
Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiambatana na Naibu
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt.
Damas Ndumbaro baada ya kutowa Heshima za Mwisho mbele ya Jeneza lenye
Mwili wa Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa la Zimbabwe Marehemu Mzee
Robert Gabriel Mugabe katika Uwanja wa Taifa wa Michezo jijini Harare
Zimbabwe. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Pombe Magufuli
kwenye Hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Rais
Ethiopya walipokutana wakati wa Hafla ya kutowa Heshima za Mwisho mbele
ya Jeneza lenye Mwili wa Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa la Zimbabwe
Marehemu Mzee Robert Gabriel Mugabe katika Uwanja wa Taifa wa Michezo
jijini Harare Zimbabwe. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John
Pombe Magufuli kwenye Hafla hiyo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
………………
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Nchi za Afrika kwa
kushirikiana na Nchi Rafiki Zimeshiriki kwa kiwango Kikubwa Sana katika
shuhuli ya kumsindikiza na kumuaga Rais wa Zamani na Muasisi wa Taifa
la Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Gabriel Mugabe.
Makamu wa Rais Mhe. Samia
ameyasema hayo leo wakati wa Shuhuli ya kuaga Mwili wa Rais wa Zamani na
Muasisi wa Taifa la Zimbabwe Marehemu Mzee Robert Mugabe iliyofanyika
kitaifa katika Uwanja wa Taifa wa Michezo Jijini Harare Nchini Zimbabwe.
Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwenye
Shuhuli hiyo ambapo alitoa Salamu za Rais kwa Wananchi na Taifa la
Zimbabwe. amesema Hotuba ya Rais wa Afrika ya Kusini Sir Ramaphoser
aliyoitowa kwa Wananchi wa Zimbabwe na Afrika kwa Ujumla ni kitendo cha
Ungwana kwa kuweza kuomba samahani kutokana na Vitendo vinavyoendelea
kufanywa wa Wananchi wa Afrika ya kusini.
Nae Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi
za Nje na Ushirikiano wa Afirka Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro amesema
Marehemu Mzee Mugabe ni kipenzi cha Wananchi wa Zimbabwe na Waafrika kwa
Ujumla hivyo hakuna budi kumuenzi na kuyaendekleza yale yote mazuri
aliyo yaacha.