RC OLESENDEKA ATENGUA KATAZO LA HALMASHAURI YA NJOMBE MABASI YA ABIRIA KUSHUSHA ABIRIA KATIKATI YA MJI


Na Amiri kilagalila-Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ameagiza mabasi ya abiria kushusha na kupakia abiria kati kati ya mji wa Njombe badala ya kutumia stendi mpya pekee hali ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wakazi wa mji wa Njombe na abiria kutokana na umbali wa stendi hiyo kutoka kati kati ya mji.

Ole Sendeka ametoa maamuzi hayo wakati akizungumza na mamia ya wananchi na wafanyabiashara katika maeneo ya stendi ya zamani na kubainisha kuwa uamuzi huo umetokana  na mashauriano na watu mbali mbali kutokana na kilio cha wananchi wa mji huo waliodai umbali wa stendi hiyo umesababisha kuongezeka kwa ghalama pindi wanapohitaji kusafiri.

“Zipo hoja ambazo tumezisikiliza kutoka kwenye halmashauri,kutoka kwa wadau,wataalamu wetu na watu mbali mbali,lakini baada ya kushauriana nimeamua yafuatayo,mabasi yote yataanzia safari na kumalizia safari katika kituo cha mabasi kikuu kilichopo mji mwema na zitalipa ushuru badala ya shilingi elfu moja zitalipa elfu mbili,lakini akishaanza kubeba abiria huko stendi atakuja hapa mwisho wa stendi ya zamani shusha au beba abiria ondoka zako nenda”alisema Ole Sendeka

Aidha Ole Sendeka ameagiza Tanlod kutengeneza kituo cha mabasi karibu na hospitali ya halmashauri ya mji wa Njombe Kibena ili kuwasaidia wagonjwa wanaofika katika hospitali hiyo huku akiahidi kushirikiana na timu yake kutafuta bajeti ya ujenzi wa vituo hivyo kwa kuwa halmashauri ya mji wa Njombe imeadai kuto kuwa na bajeti hiyo.

Baadhi ya wakazi wa Njombe akiwemo Onesmo Mwajombe na Rose Mayemba waliohudhulia katika mkutano huo wamepongeza maamuzi hayo na kwamba itawasaidia kupunguza gharama pindi wanaposafiri kwa kuwa kilikuwa kilio chao cha muda mrefu.

“Tuna shukuru sana sana kwa kusikilizwa kilio chetu lakini kwa kuwa mkuu wa mkoa ametetea wanyonge wengi tulio kuwa tunalia juu ya adha hii”alisema Onesmo Mwajombe

Aidha katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya mji wa Njombe kilichofanyika wiki kadhaa zilizopita kiliazimia kutokuwa na vituo vya kushusha na kupakia abiria wanaotoka na kuingia katikati ya mji huo,zaidi ya kutumia stendi mpya na maeneo yaliyopendekezwa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post