Mfanyabiashara
Mohamed Dewji ‘Mo’ ameibua mjadala mtandaoni baada ya kuweka ujumbe
uliowaibua wachangiaji kukumbushia tukio la kutekwa kwake.
Septemba 17, 2019 , Mo aliweka ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter akisema, “Kuna maisha ya mtandaoni na maisha halisi.”
Ujumbe
huo umejadiliwa kwa mitizamo tofauti huku wengine wakikumbushia
alivyotekwa na watu wasiojulikana jinsi watu walivyotumia mitandao hiyo
kupaza sauti zao.
Mmoja wa watu waliojadili ujumbe huo ni mwanaharakati Maria Sarungi Tsehai alieandika “Bring Back Mo ilikuwa maisha ya mtandaoni au maisha halisi? Tutaelewana Tu”
MO Dewji baada ya kuona hivyo akaamua kuomba msamaha “Nisamehe
sana dada yangu. Naona umeichukulia tweet yangu out of context. Narudia
kuwashukuru wote ambao mliniombea ne kunisemea”.
Msanii Lady Jay Dee akichangia ujumbe huo amesema, “Nadhani
(Mo) alimaanisha watu wanaoishi maisha ya uongo kuonyesha vitu ambavyo
hawana katika maisha yao halisi. Hasa watu wengi maarufu wana hizo sana.
Hata kupigia picha juice ambayo sio yako na kui post nayo ni maisha ya
mtandaoni"