TANAPA kwa kushirikiana na hifadhi ya ziwa manyara watoa elimu kwa vijiji 25



Na Queen lema
 
shirika la hifadhi la taifa (TANAPA)kwa kushirikiana na hifadhi ya ziwa manyara limefanikiwa kutoa elimu kwa vijiji 25 kuhusiana na masuala mbalimbali ya matumizi bora ya ardhi ikiwa ni pamoja na namna ya kuendelea kuhifadhi na kulinda ziwa hilo.

Akiongea jana na wataalamu wa masuala ya sayansi na mazingira ambao walitembelea hifadhi ya ziwa hilo la manyara Bi Noelia myonga ambaye ni kamishana msaidizi wa hifadhi ya ziwa hilo alisema kuwa elimu hiyo imetolewa kwa vipindi tofautitofauti.

kamishna alisema kuwa elimu hiyo ilitolewa ililenga kwa vijiji vya jirani ambavyo vinazunguka hifadhi ya ziwa hilo ambapo pia imelenga kuokoa ziwa hilo ambalo bado linaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa hasa ya shuguli za binadamu.

Aidha ametaja changamoto amazo bado mpaka sasda zinakabili ziwa hilo kuwa ni pamoja na kujaa tope ambalo linasababisha hata kina cha ziwa hilo kuendelea kupungua siku hadi siku tofauti na hapo awali ambapo kina cha ziwa hilo kilikuwa kirefu sana.

kamishna Noelia amedai kuwa ziwa hilo linajaa matope kutokana na baadhi ya wanakijiji kuendelea kufanya shuguli kama kilimo na uufugaji kwa kutegemea vyanzo vya mito hali ambayo hufanya matope na maji yote kurudi katika ziwa hilo na kisha kugeuka matope.

Kutokana na hali hiyo amewaoamba wataalamu kwa kushirikiana na wizara mbalimbali kuendelea kujikita zaidi kwenye kutoa elimu ambayo inalenga zaidi kuyatunza na kuhifadhi ziwa hilo kwa ajili ya wanyama lakini hata vizazi vijavyo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post