Aliyekuwa
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema hatarejea
Tanzania Septemba 7, 2019 kama ilivyopangwa badala yake atasubiri ruhusa
ya madaktari wanaomtibu.
Lissu
ametoa kauli hiyo jana Jumanne Septemba 3, 2019 katika mahojiano na
Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC), alipoulizwa lini atarejea
Tanzania.
Amesema bado madaktari hawajaweka bayana kwamba atarudi lini.
"Nilisema mwanzoni nitarudi tarehe 7 Septemba, 2019 lakini daktari wangu ameniambia ataniona tarehe 1 Oktoba, 2019 na mara ya mwisho ataniona mara ya mwisho tarehe 8 Oktoba, 2019, kwa hiyo ile ratiba ya mwanzo haitawezekana, kwa sababu daktari wangu anataka kuniona." amesema Tundu Lissu

Lissu,
amekuwa nje ya nchi tangu Septemba 7, 2017 aliposhambuliwa kwa risasi
zaidi ya 30 na watu wasiojulikana akiwa eneo la makazi yake Area D,
Dodoma akitoka kuhudhuria vikao vya Bunge.