WAZIRI WA KILIMO JOSEPHAT HASUNGA AKUTANA WAZIRI WA KILIMO NA WAZIRI WA MAENDELEO VIJIJINI WA ISRAEL

Na Mathias Canal, Bet Dagan-Israel

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) tarehe 5 Septemba 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen na kukubaliana kwa kauli moja kuwa serikali za nchi hizo mbili kuingia makubaliano ya kuendeleza kilimo hususani katika utafiti, Tija katika uzalishaji, na Teknolojia.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Balozi wa Tanzania nchini Israel Mhe Job Daud Masima, Mhe Hasunga ametoa shukrani kwa Serikali ya Israeli kuipatia Tanzania nafasi 100 za kujifunza kuhusu sekta ya kilimo kwa vijana kupitia programu inayosimamiwa na Agrostudies.

Waziri Hasunga ameeleza katika mkutano huo dhamira ya Serikali ya Tanzania inayoongoza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli, ya kuwasaidia vijana waliorudi nyumbani baada ya mafunzo hayo kwa kuanza kuwapatia mahitaji ya msingi ikiwemo ardhi ambayo ipo eneo litakalowawezesha kujiendeleza.

Vilevile ameeleza kuwa katika wizara ya kilimo hakukuwa na kitengo cha masoko hivyo ili kuwaunganisha vijana hao na masoko ya biashara watakazozalisha serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Kilimo imeanzisha kitengo maalumu cha kushughulikia masoko ya mazao mbalimbali ya wakulima.

Waziri Hasunga pia amezungumzia kuhusu maeneo yanayoweza kuwavutia wawekezaji kutoka Israeli ili kuwekeza nchini Tanzania kwa kutoa takwimu za ukubwa wa ardhi yenye rutuba, uwepo wa maji na hali ya hewa inayoruhusu ukuaji wa aina nyingi ya mazao.
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen, mkutano huo umefanyika Mjini Bet Dagan 50250 nchini Israel tarehe 5 Septemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.

Waziri wa Kilimo wa Tanzania Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa Israel Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi za wizara hiyo eneo la Bet Dagan 50250 nchini Israel, tarehe 5 Septemba 2019.

Serikali ya Israeli ipo tayari kusaini hati ya makubaliano ya kilimo (Memorandum Of Undarstanding-MOU) ya kilimo pale itapowasilishwa na Serikali ya Tanzania, hii imekuja baada ya Mheshimiwa Waziri Hasunga kuona umuhimu wa kuingia makubaliano ili iwe rahisi wawekezaji kutoka Israel kuzuru Tanzania kuwekeza pamoja na kupata mikopo kutoka katika Serikali yao.

Akizungumza kwa niaba ya Serikali ya Israeli Waziri wa Kilimo na Maendeleo Vijijini wa nchi hiyo Mhe Uri Yehuda Ariel HaCohen imehaidi pindi Serikali ya Tanzania itakapowasilisha mahitaji hasa kwenye mazao ambayo muhimu ya kuanza nayo kwa ajili ya soko la Israel itakuwa tayari kushirikiana kwa kutoa ujuzi pamoja na uwezeshaji wa wataalamu.

Hata hivyo itakapotokea mwekezaji wa Israeli ataposhirikiana na kampuni ya Tanzania, Serikali inawajibu kuingilia kati kusaidia maeneo ya uwezeshaji na rasilimali watu.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post