Elimu ya Mpiga Kura ipo mkoani Tabora kabla ya Uboreshaji wa Daftari Oktoba 14-20, 2019


Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari Daniel Kasokola akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tabora Boys (Tabora School) wakati Gari la Matangazo la NEC lilipotembelea shule hiyo iliyopo Mjini Tabora kutoa Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Tabora, Katavi, Rukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma unaotarajiwa kuanza Oktoba 14 hadi Oktoba 20, 2019.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) upande wa Habari Daniel Kasokola, akieleza jambo mbele ya mwanafunzi mwenye ulemavu wa macho wa Shule ya Sekondari Tabora Boys Elisha John kuhusu kipaumbele ambacho NEC inakitoa kwa makundi maalum wakiwemo watu wenye ulemavu.
Gari la Matangazo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi likiwa kwenye Shule ya Sekondari ya Tabora Boys (Tabora School) iliyopo Mjini Tabora kutoa Elimu ya Mpiga Kura kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Tabora, Katavi, Rukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma unaotarajiwa kuanza Oktoba 14 hadi Oktoba 20, 2019.
Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Moshi Makuka akitoa Elimu ya Mpiga Kura kwenye Soko la Isevia lililopo Mjini Tabora kuelekea Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Tabora, Katavi, Rukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma unaotarajiwa kuanza Oktoba 14 hadi Oktoba 20, 2019.
Afisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Monica Wabukundi (kushoto) akitoa Elimu ya Mpiga Kura kwa wafanyabiashara wa Soko la Isevia la Mjini Tabora kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mkoa wa Tabora, Katavi, Rukwa na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma unaotarajiwa kuanza Oktoba 14 hadi Oktoba 20, 2019.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post