Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Aggrey & Clifford, Ibrahim
Kyaruzi, akipokea tuzo kwa niaba ya kampuni kutoka kwa Mkurugenzi wa
kampuni ya Bankable Tanzania Limited Lawrence Mafuru (Kushoto).
Kampuni ya matangazo na ukuzaji masoko ya Aggrey & Clifford, kwa
mara nyingine imepata tuzo kutokana na kuwa miongoni mwa makampuni 100
ya kati yanayofanya vizuri kibiashara.
Kampuni ya Aggrey & Clifford ambayo hivi karibuni ilisherehekea
miaka kumi tangu kuanzishwa kwake, ilitunukiwa tuzo hiyo mwishoni mwa
wiki jijini Dar es Salaam kwenye hafla fupi iliyofanyika Serena Hotel.