NCHI ZA SADC ZASUASUA KURIDHIA ITIFAKI YA MAZINGIRA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Malisili na Utalii ,Prof ,Adolf Mkenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Makatibu wakuu na Maafisa Waandamizi wa Sekta za Mazingira ,Malisili na Utalii kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo , kusini mwa Afrika (SADC) .

 

Na Claud Gwandu,Arusha
PAMOJA na athari za mabadiliko ya tabianchi kuzikumba nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa  Afrika(SADC),nchi hizo bado zinasuasua kuridhia itifaki ya utunzaji wa mazingira, miaka mitano tangu ilipopitishwa.
 Itifaki hiyo pamoja na mambo meingine,ina malengo ya kuhifadhi mazingira kwa ajili ya maendeleo endelevu na ilipitishwa mwaka 2014 na Kikao cha wakuu wa nchi  wa Jumuiya hiyo yenye wanachama nchi 16.
 Hadi sasa ni nchi tatu tu kati ya 16 zilizoridhia itifaki hiyo ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini,Msumbiji na Zambia huku Tanzania ikielezwa kuwa katika hatua za mwisho za mchakato wa kuridhia itifaki hiyo.

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu  wa Rais(Mazingira),Joseph Malongo amesema hayo jijini hapa leo katika ufunguzi wa mkutano wa Makatibu wakuu wa nchi za SADC wanaoshughulikia na sekta za Mazingira,Maliasili na Utalii.

Amesema kuwa katika mkutano huo ambao ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wanaosimamia sekta hizo katika nchi wanachama, watajaribu kushawishi nchi wanachama waridhie itifaki hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa kutokana na nchi hizo kushirikiana katika kutunza rasilimali zinazovuka mipaka kati ya nchi nan chi.

“Pamoja na kwamba kikao cha viongozi wakuu kilipitisha itifaki hii mwaka 2014,ni nchi tatu tu zilizoridhia itifaki hii muhimu hasa ikizingatiwa katika masuala ya mazingira tuna share resources (Tunashirikiana katika masuala mengi ya rasilimali)  nyingi sana,mfano Ziwa Tanganyika lipo Tanzania,Jamhuri ta Kidemokrasia ya Congo,Mto Zambezi ambao unapita katika nchi kama tano za SADC.

 “Kwa hiyo kuna umuhimu wa kukaa pamoja na kuangalia namna bora ya kutunza, kwa pamoja, mazingira  yanayozunguka rasilimali hizo kwa ajili ya maendeleo endelevu ya nchi wanachama na Jumuiya,” alisema Katibu Mkuu huyo.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano huo Profesa Adolf Mkenda ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii anasema mkutano huo utajadili mambo mengi ikiwamo kupambana na ujangili, mkataba wa kimataifa wa kulinda viumbehai na mimea iliyo katika hatari ya kutoweka(CITES) ambao unakataza na kuruhusu uuzaji wa nyara zinazotokana na wanyamapori.

”Tunakutana kujadili  mambo mengi kuhusu mazingira,maliasili na utalii hasa ushirikiano katika mapambano dhidi ya ujangili pamoja na kuandaa ajenda kwa ajili ya mkutano wa mawaziri wa sekta hizo wa SADC ambao utafanyika hapa, “anasema Profesa Mkenda

Aliongeza kuwa katika mkataba wa CITES kuna mjadala mkubwa unaoendelea miongoni mwa wadau ambapo baadhi ya vipengele vinaonekana kuchomekwa  kinyume cha utaratibu,hivyo mkutano huo utajadili na kutoa mapendekezo ya vipengele hivyo
 “Kwa mfano kuna mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) yanayotumika kupiga kampeni ya kuzuia uvunaji halali wa mazao ya wanyamapori na kupinga bidhaa kuingia sokoni jambo ambalo tunadhani si sahihi,na hilo ni moja ya maeneo tutakayoyajadili na kuyatolea mapendekezo,” alisisitiza Profesa Mkenda
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kilimo,Chakula na Maliasili katika Sekretarieti ya SADC, Domingos Gove,amesema Mkutano huo ni wa kikatiba na wa kawaida unaofanywa na wataalamu mbalimbali katika nchi za SADCkwa ajili ya kujadili changamoto na mafanikio yaliyorifikiwa nan chi wanachama

Mkutano wa Mawaziri wa sekta za Mazingira,Maliasili na Utalii wan chi wanachama wa SADC utafunguliwa ijumaa wiki hii na Makamu wa Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Hassan Suluhu

Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifutilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf Mkenda (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho .
Mkurugenzi wa Idara ya Chakula ,Kilimo na Maliasili wa  Sekretarieti ya SADC ,Domingos Gove akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo unaoshirikisha Makatibu Wakuu kutoka nchi 16 za SADC.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano huo wakifutilia hotuba iliyokuwa
ikitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ,Prof Adolf
Mkenda (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao hicho .
Baadhi ya Makatibu Wakuu wanaoshiriki Mkutano huo. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,prof ,Adolf Mkenda akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa Makatibu Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za SADC.
Mkurugenzi wa Idara ya Chakula ,Kilimo na Maliasili wa Sekretarieti ya SADC,Domingos Gove akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa
Makatibu Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za
SADC. 

  Katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira ,Joseph Malongo akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufunguliwa rasmi kwa mkutano wa
Makatibu Wakuu wa Wizara za Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za
SADC.
Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi  wa Sekta ya Mazingira,Maliasili na Utalii wa nchi za SADC ,wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mkutano huo unaofanyika kituo cha kimataifa cha Mikutano cha AICC jijini Arusha.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post