RC MNYETI AZINDUA BARABARA ZA KITETO

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akizungumza baada ya kuzindua mojawapo ya barabara za Wilaya ya Kiteto.
Meneja wa Wakala wa barabara wa Mijini na Vijiji (TARURA) Wilaya ya Kiteto mhandisi Edwine Magiri (kushoto) akizungumza baada ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti (katikati) kuzindua mojawapo ya barabara za eneo hilo.
……………….
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amezindua barabara za Wilaya ya Kiteto za urefu wa kilomita 19.14 zilizotengenezwa kwa gharama ya shilingi 380,883,000.
Meneja wa wakala wa barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilaya ya Kiteto mhandisi Edwine Magiri akizungumza baada ya RC Mnyeti kuzindua barabara hizo alisema zimefanyiwa matengenezo kwa kuanzia April 2019 hadi Julai 2019. 
Mhandisi Magiri alisema kati ya barabara hizo kilomita 19.14 zimewekewa changarawe na nyinginezo zimefanyiwa ukarabati wa kawaida. 
Alisema katika ujenzi wa kilomita hizo za barabara hizo kumewekewa na kujengewa kalvati 22 na pia kumejengwa madrifti mawili. 
“Kazi zimefanyika kwa wakati na kiwango kinachotakiwa ikiwemo vipimo kwani tulisimamia ujenzi ipasavyo wakati wa shughuli hiyo,” alisema mhandisi Magiri. 
Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti akizungumza wakati akizindua mojawapo kati ya barabara hizo aliwapongeza Tarura Kiteto kwa namna walivyotengeneza barabara hizo. 
Hata hivyo, Mnyeti alitoa wito kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa barabara kuwa na tabia ya kusafisha mazingira ili ziwe safi kwa kuondoa uchafu. 
“Kuna ule utaratibu wa kufanya usafi kila mwisho wa mwezi, tumieni nafasi hiyo kwa kuhakikisha mnaondoa uchafu uliopo pembezoni hasa katika mitaro,” alisema Mnyeti. 
Pia, Mnyeti aliipongeza Tarura na wakala wa barabara za nchini (Tanroads) mkoani humo kwa namna wanavyotengeneza barabara na kuzikarabati pindi kukitokea matatizo. 
“Ukipita Manyara unakuta barabara zake zinapitika bila shida hongereni kwa hilo kwani ukipita sehemu nyingine unaona changamoto kwa wenzetu namna barabara zao zilivyo,” alisema Mnyeti. 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post