Miradi ya maji bado ni kichefuchefu wilayani Bunda

Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza katika mkutano

Naibu Waziri Jumaa Aweso akikagua mradi wa maji Wilayani Bunda Mkoani Mara

ASHA SHABANI MARA.
Naibu waziri wa maji Jumaa Aweso amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kufika wilayani Bunda Mkoani Mara na kukagua maendeleo ya miradi ambayo utekelezaji wake ni mbovu kiasi chammirafi hiyo kumaliza miaka zaidi ya Saba miradi haujakamilika.

Miradi ambayo utekelezaji wake ni wa kusuasua kutokana na wakandarasi wa miradi hiyo kuwa Nina ya muda huku utekelezaji wak ukiwa chini ya kiwango ni mradi wa  Kinyambwiga , Nyabheho ,nyangaranga pamoja na mradi wa Maji mugeta.


Akizungumza baada ya kujionea jinsi wakandarasi wa miradi hiyo wanavyo itekeleza kiwango kisicho ridhisha naibu waziri wa maji Juma Aweso amemtaka katibu mkuu wa wizara hiyo kufika na kuvunja mikataba yao kutokana na kusua sua katika kazi hiyo.

Aidha Aweso amesema kuwa miradi yote inayotekelezwa wilayani Bunda mkoani Mara ni Kichefu chefu kutokana na kutokusimamiwa vema na watendaji wa serikali ambao wapo wanaina madudu ya wakandarasi lakini wamekuwa wakiedelea kuwapa mikataba mingine .

Awali wananchi katika kijiji cha Kinyambwiga wakizungumzia juu ya mwenendo wa mkandarasi wa mradi wao ameshindwa kazi kwani  miradi huo ulikuwa wa muda mfupi lakini wanshanga kuona umemaliza miaka sita sasa bila kukamilika.

Miradi ya maji ya Kinyambwiga na Nyabheho inagharimu zaidi ya shilling Billioni kumi na million mia tisa ili kujengwa chujio na usambazaji wa maji  huku mradi wa maji wa nyangaranga na mgeta umegarimu zaidi ya milioni 9.15 kwa ajili ya kuwapatia  wananchi wilayani humo maji.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post