TAKUKURU KUMPANDISHA KIZIMBANI HAKIMU KWA TUHUMA YA KUPOKEA RUSHWA

Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Hussein Mzee Mussa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Shinyanga inatarajia kumfikisha Mahakamani Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Kishapu Benjamin Charles Mhangwa kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa kinyume cha kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa Na 11 ya Mwaka 2007.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Oktoba 9,2019 Kaimu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Hussein Mzee Mussa amesema hakimu huyo aliomba na kupokea kiasi cha shilingi 200,000 kati ya shilingi 300,000/= alizoomba kutoka kwa Juma Mbugi kuwa ametumwa na hakimu wa wilaya ya Kishapu Wilberforce Luwago ili kusaidia kupata ushindi katika kesi ya kubakwa kwa mwanawe.

Aidha kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika umebaini kuwa fedha hizo hazikuombwa na hakimu Mkazi Mfawidhi wa wilaya ya Kishapu Wilberforce Luwago hivyo mtuhumiwa huyo aliomba na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.


This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post