wachezaji wa timu ya simba wakifurahia goli dhidi ya Singida United leo katika uwanja wa kumbukumbu ya marehemu Shekh Amri Abeid Jijini Arusha |
Na.Mwaandishi wetu,Arusha
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara
Simba wameendelea kukusanya alama tatu baada ya kuichapa bao 1-0
Singida United leo kwenye Uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Simba huu ni mchezo wao wa Sita
wakicheza bila kupoteza hata mechi moja wakifikisha jumla ya alama 18 na
kuendelea kukalia usukani wa Ligi hiyo.
Simba walipata bao na la ushindi
kwao kupitia kwa Mshambuliaji Kinda Miraji Athuman “Sheva’ mnamo dakika
ya 41 kipindi cha kwanza.