YANGA HOI CCM KIRUMBA YACHAPWA 2-1 NA PYRAMIDS YA MISRI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Manahodha wa timu ya Yanga na Pyramids ya nchini Misri wakiwa katika picha ya pamoja na waamuzi wa mchezo dhidi ya timu hizo kuwania nafasi ya kuingia kwenye makundi kombe la  shirikisho barani Afrika
Na.Mwaandishi Wetu,Mwanza

Timu ya Yanga imejiweka katika mazingira magumu ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 na Pyramids FC kutoka Misri mchezo uliopigwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Wageni walikuwa wa kwanza kuandika bao kupitia kwa kiungo mshambuliaji raia wa Burkina Faso ,Eric Traory dakika ya 42 baada ya kuachia shuti ndani ya box na kumuacha Shikalo hana la kufanya.

Hadi  zikwenda mapumziko timu ya Kizazi kipya toka Misri ilikuwa mbele kwa kuongoza bao moja kwa bila.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kufanya mabadiliko hata hivyo wageni walinufaika na mabadiliko hayo dakika ya 62 Nahodha wa Pyramids FC ,Abdallah  Saied alifunga bao la pili.

Hata hivyo Yanga walipata bao la kuvutia machozi dakika ya 88 likifungwa na Nahodha Papy Tshishimbi na mnamo dakika ya 90 Yanga walipata pigo kwa beki wao kisiki Kelvin Yondani kuonyeshwa kadi Nyekundu.

Kwa matokeo hayo timu Pyramids FC imejiweka katika mazingira ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza wakiwa na mabao mawili ya ugenini hivyo Yanga wanatakiwa kwenda kushinda jumla ya mabao 2-0 ili waweze kupindua matokeo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post