WANAWAKE WATAJWA KINARA WA KUFANYA BIASHARA ZA MTANDAONI, JUKWAA LA UTAWALA WA MTANDAO TANZANIA(IGF) LAWEKA TAFITI HADHARANI



Na Seif Mangwangi, Arusha

WANAWAKE wametajwa kuwa vinara wa matumizi ya mitandao kufanya biashara (e-business), duniani ikiwa ni mara mbili zaidi ya wanaume.
Mratibu wa Kamati ya Jukwaa la Utawala wa Mtandao(IGF) Nazar Nicholas,  Nazar Nicholaus akiwasilisha mada katika kongamano la siku moja linalofanyika jijini Arusha kuhusu masuala ya mtandao.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 16, 2019 wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Utawala wa Mtandao Tanzania (IGF), linalowakutanisha wadau, taasisi za Serikali na asasi mbalimbali za kiraia kujadili mafanikio na changamoto zinazotokana na matumizi ya mtandao.

Akizungumza  katika ufunguzi wa kongamano hilo linaloendelea jijini Arusha, Mtaalam wa masuala ya mtandao na mkufunzi katika chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Profesa Eliamani Sedoyeka amesema kasi ya matumizi ya biashara mtandao imekuwa kubwa sana katika miaka ya karibuni tofauti na hapo awali.
Mtaalam wa Masuala ya mtandao ambaye pia nia Mhadhiri kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Profesa Eliamani Sedoyeka akizungumza wakati akifungua kongamano la wadau wa mtandao linaloendelea jijini Arusha.

Amesema katika utafiti alioufanya mwaka jana nchini, aliweza kugundua kuwa wanawake wamekuwa wakitumia fursa za uwepo wa mitandao katika kutangaza, kununua na kuuza kwa njia ya mitandao mara mbili Zaidi ya wanaume.

Profesa Sedoyeka kupitia kongamano hilo ametoa mwito kuwataka watumiaji wa mitandao kuitumia katika njia salama ili kuepuka kutapeliwa hususani kwa wanaotumia kwa ajili ya kufanya biashara.
Washiriki wa Jukwaa la utawala mtandaoni Tanzania kutoka maeneo mbalimbali nchini wakiwa katika picha ya pamoja, wa tatu kutoka kulia ni mtaalam wa TEHAMA na mhadhiri wa Chuo Cha Uhasibu Arusha Profesa Eliamani Sedoyeka aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kongamano hilo 



Washiriki wakimsikiliza mtoa mada Mratibu wa Jukwaa la utawala mtandano Tanzania, Azar Nicholaus (Hayupo pichani). 

Hata hivyo amesema mtandao kama rasilimali muhimu bado haitumiki vizuri kwani kuna tatizo la baadhi ya watumiaji kutoamini kama njia sahihi ya kufikisha ujumbe na ndio maana baadhi ya watu wakitumiwa barua kwa njia ya mtandao lazima watapiga simu kwaajili ya kuhakiki.

Amewataka watumiaji wa mtandao kuweka nywila (password), ili kuepuka watu wanaotumia vibaya mitandao kwa kufanya uhalifu na kwamba endapo utapenda kumpatia mwenza wao nywila hiyo lakini lazima kuhakikisha simu au kompyuta imewekwa nywila.

Kwa upande wake Mratibu wa Kamati ya Jukwaa la utawala mtandao Tanzania, Nazar Nicholaus, amesema  matumizi ya mtandao yamekuwa na changamoto kubwa sana ambapo watu wamekuwa wakiitumia vibaya bila kujua athari za baadae.

“Tumekuwa tukifuatilia yanayoendelea mtandaoni, bado kuna baadhi ya watu wanaitumia vibaya na wengine kutoa taarifa ambazo si sahihi.Kwa mfano hivi karibuni kuna mtu aliamua kutumia mtandao kutoa taarifa za kwamba mmoja ya Waziri Mkuu mstaafu nchini (akamtaja) amefariki dunia wakati sio kweli.Kuna mifano mingi tu ya matumizi yasiyo sahihi.

“Ni jukumu la kila moja wetu kuhakikisha tunaitumia mitandao vizuri na ukweli uliopo katika mitandao kuna mambo mengi yenye tija Zaidi kwa maendeleoe ya nchi yetu.Mtandao ni zakidi ya kutuma picha katika Whtsap na facebook, hiyo ni sehemu ndogo sana na tunaweza kusema kama ni asilimia basi ni 0.0001,”amesema Nicholas.

Kuhusu kongamano ambalo limewakutanisha wadau hao Nicholas amesema IGF inatambua umuhimu wa kuwakutanisha wadau wa masuala ya mtandao kwa ajili kukaa pamoja kujadiliana na kubadilisha mawazo kuhusu njia bora ya kutumia mtandao na hivyo anaamini kupityoia kongamano hilo watatoka na mawazo yaliyo bora.

“IGF tutaendelea kuwakutanisha wadau wa mtandao kwa ajili ya kujadiliana kwa pamoja.Tulikuwa tumesinzia kidogo lakini sasa tumeamka na binafsi niliamua kuchukua jukumu la kuhakikisha wadau wanakutana.
amesema Nicholas.

Kuhusu nafasi ya watu wenye mahitaji maalumu wakiwamo wenye ulemavu kushirikishwa katika IGF, Nicholas amesema kwa kutambua nafasi yao imekuwa ikiwashirikisha na hata kwenye kongamano linaloendelea wameshirikishwa kikamilifu na mawazo na maoni yao yatapewa kipaumbele.

Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karasan ambao ni miongoni mwa wafadhili wa kongamano hilo amewataka wanawake kutumia nafasi ya kuwa vinara kimataifa kuanzisha njia za mawasiliano za kimtando ili kujipatia fedha.

Amesema kutokana na mabadiliko ya teknolojia, watu wengi wanaweza kufanya biashara ya redio mtandaoni, televisheni na hata blogs ambazo zitaweza kuwaingizia fedha nyingi kupitia matangazo watakayokuwa wakiyatangaza kupitia mitandaoni.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post