TASAF YALETA MATOKEO CHANYA NJOMBE


Na Mwandishi Wetu, APC BLOG, NJOMBE 
 
Mpango wa kunusuru kaya masikini nchini Tanzania TASAF unaofadhiliwa na shirika la kimataifa la mafuta OPEC umetajwa kubadili maisha ya wanufaika wengi katika Halmashauri ya mji wa Makambako Mkoani Njombe.

Imeelezwa kuwa hapo awali wananchi wengi wa Makambako walikuwa wakiishi maisha duni lakini baada ya kupatiwa msaada huo hivi sasa wameenda katika kipato cha kawaida na wanaishi maisha mazuri kupitia msaada wa fedha kuendesha miradi ya kilimo, ufugaji n.k


Baadhi ya wanufaika ambao wameweka bayana mafanikio waliopata na kukiri kubadilika kimaisha Ni pamoja na Amon Kidenya na Salome Mligo ambao walipewa fedha na kuanzisha mradi wa ufugaji wa ng’ombe na kuku na kufanikisha ujenzi wa nyumba ya kuishi huku mwingine akidai amekuwa na uhakkika wa kupata milo zaidi ya mitatu.

Akifafanua namna mpango wa TASAF ulivyofanikiwa kutekeleza miradi 48 yenye thamani ya bil 1.9 katika awamu ya kwanza inayotekelezwa katika kipindi cha miaka 5 kwa kushirikiana na wananchi wanaochangia asilimia 10 katika utekelezaji wa baadhi ya miradi mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Makambako Paul Malala amesema ujio wa mpango huo umekuwa na matokeo makubwa chanya kwa wananchi na serikali.

Malala amesema TASAF imefanikiwa kujenga vituo vya afya 3 ,barabara 7 ,mabweni 5 ,madarasa 6 ofisi za walimu 2 na miradi mingine ya ufugaji na kilimo Cha parachichi na mbao.

Wanafunzi nao akiwemo Amosy Makinge na Sabrina Sanga  wanaeleza jinsi mpango huo ulivyosaidia kuboresha miundombinu ya elimu kwa kujenga mabweni,darasa na vyoo na kurahisisha upatikanaji wa elimu bora.

Lakini mafanikio yamekujaje kwa wanufaika mjini Makambako ambao waliingizwa kwenye mpango wakiwa hawana uhakika wa mlo hata mmoja na kusomesha watoto na kufanikiwa kupiga hatua kubwa kiuchumi na kulazimika kupisha wengine wenye hali mbaya. Hapa mratibu wa TASAF Makambako Veronica Simwanza anaeleza jitihada zilizochukuliwa.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post