Na Mwandishi Wetu Dar es Salaam
Bodi
ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali nchini imeliagiza Baraza
la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kukutana ili kuhakikisha
wanatatua changamoto za uendeshaji wa Baraza hilo kikamilifu na kutoa
taarifa kwa Bodi ndani ya siku 14 jinsi walivyoshughulikia changamoto
hizo, ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Baraza
hilo.
Agizo
hilo limetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi hiyo
Dkt. Richard Faustine Sambaiga wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza
la Taifa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kikao kilicholenga
kutoa maelekezo mahsusi kwa Baraza ili kukitaka chombo hicho kuzingatia
matakwa ya kisheria katika uendeshaji wake.
Dkt.
Sambaiga ameliagiza Baraza hilo kufanya mapitio ya Kanuni ya Sheria ya
marekebisho Na. 11/2005 na Sheria ya marekebisho Na.3/201 ili kuweza
kukidhi mapendekezo ya mapitio ya Kanuni hizo na kuwasilisha kwenye Bodi
ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali ndani ya siku 30 ili kuondoa mkwamo
wa kiutendaji wa majukumu ya Baraza la NGOs nchini.
Pia
Dkt. Sambaiga ameliagiza Baraza hilo kujielekeza kwenye matakwa ya muda
wa kisheria wa kuwa kiongozi wa Baraza hilo ambao ni miaka mitatu toka
kuteuliwa kwa Baraza mwaka 2016, na hivyo kuelekeza kuanza kwa mchakato
wa uchaguzi wa Baraza jipya ndani ya siku 30.
“Nalielekeza
Baraza kupitia upya uwakilishi wa wajumbe wa Mikoa na makundi maalum
hasa ikizingatiwa ipo Mikoa mipya na makundi ambayo hayana wawakilishi
kwani kumekuwa na changamoto kubwa ya uwakilishi wa wajumbe kutoka
mikoani” alisema.
Aidha
Dkt. Sambaiga amewataka Viongozi wa Baraza la Taifa kuzingatia
uwasilishaji wa taarifa yake ya utekelezaji wa kazi zake kwa Bodi ili
kutosababisha Bodi kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kisheria kama
yalivyoainishwa kwenye kifungu 7(1) (j) cha Sheria ya Mashirika yasiyo
ya Kiserikali kinachoitaka Bodi kupokea kujadili na kupitisha taarifa za
Baraza hilo.
Dkt.
Sambaiga amelitaka Baraza kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria
ikiwemo kutetea maslahi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kuwa
jukwaa la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali na kuhakikisha wanakuwa mwavuli
wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika masuala yote yanayohusu
uratibu na kutandaa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali; na
“Nawasihi
viongozi wa Baraza Kutunga na kusimamia utekelezaji wa Kanuni za
Maadili kwa lengo la kuwezesha Mashirika Yasiyo ya kiserikali kujiongoza
kwa kufuata misingi ya kimaadili yenye uwazi na uwajibikaji.”
Mweyekiti
wa Bodi ya Mashirika Yasika ya Kiserikali ameleza kuwa maelekezo
anayoyatoa yanalenga kuhakikisha kuwa Baraza la Mashirika ya NGOs
linatekeleza kazi zake kikamilifu, kuimarisha uratibu wa sekta ya NGOs,
kuondoa chanagmoto za uendeshaji wa NGOs hivyo Bodi ikalazimika kutoa
maagizo thabiti kuboresha uendeshaji wa kazi za NGOs nchini.
Dkt
Simbaiga amelieleza Baraza la Taifa la NGOs kuwa ulegevu wa kiutendaji
ndani ya Baraza la NGOs unakwamisha utendaji wa kazi za Bodi ya NGOs
amabzao wamekasimiwa kuzitekeleza kwa mujibu wa sharia, kanuni na
taratibu.
Naye
Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Bw. Nicolaus
Zachariah ameshukuru kwa hatua iliyochukuliwa na Mwenyekiti wa Bodi ya
NGOs ya kukutana na wajumbe wa Baraza la NGOs na kujadili masuala yenye
chanagamoto katika uendesjai wa majukumu ya Baraza. Baraza la NGOs
limepokea maelekezo ya Bodi na kukiri kuyafanyia kazi maagizo yote kwa
pamoja kama yalivyowasilishwa na Bodi ya NGOs.
Aidha,
Baraza la NGOs limeaomba kuendelea kupata ushauri wa kitaalam na msaada
wa kisheria ili kuhakikisha kuwa maalekezo yote yanatekelezwa katika
muda uliokubainishwa.
Bodi
ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali iliyoanzishwa chini ya
Kifungu cha 6 (1) cha Sheria ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya
Mwaka 2002 kwa lengo la kuwakilisha Sekta ya Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali ikiwa na jukumu la kusimamia uratibu wa Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali nchini ikiwemo uendeshaji wa Baraza la Taifa la Mashirika
Yasiyo ya Kiserikali.