Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera John Joseph akitoa elimu ya rushwa ya ngono kwa waandishi wa habari mkoani Kagera.
Na Ashura Jumapili - Malunde 1 blog Bukoba
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania (TAKUKURU )
imeanzisha kampeni ya kitaifa ya" vunja ukimya kataa rushwa ya ngono
"ili kutoa fursa kwa waathiriwa wa matatizo ya ngono kufunguka.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera John
Joseph,wakati akitoa elimu ya rushwa ya ngono kwa waandishi wa habari
mkoani humo.
Joseph alisema rushwa ya ngono inamdhalilisha mtu,inasababisha magonjwa
maana unaweza kujikuta unashiriki ngono na mtu ambaye ana magonjwa ya
kuambukiza na kumuambukiza mwingine.
Alisema upo ulazima wa nchi na wadau mbalimbali kushirikiana ili kuweza kufichua vitendo vya rushwa ya ngono katka jamii.
Alisema matukio ya rushwa ya ngono yanafanyika kwa wingi lakini
hayaripotiwi katika mamlaka husika ili ziweze kuchukua hataua stahiki.
Alisema zaidi ya matukio 391 yaliripotiwa takukuru ya kuombwa
rushwa ya Ngono hapa nchini kwa mwaka 2017 Hadi 2019 na majalada 46
yalifanyiwa uchunguzi.
Alisema kuwa Takukuru Mkoa wa Kagera unampango wa kuanzisha dawati
amaalumu la Rushwa ya Ngono ili jamii iweze kutambua madhara yatokanayo
na rushwa ya ngono.
"Nitumie nafasi hii kuwajulisha jamii na jinsi Rushwa ya Ngono jinsi
inavyo mdhalilisha mtu na inasababisha magonjwa maana huwezi jua kuwa
yule anayefanya Jambo Hilo kuwa ni mgonjwa au la",alisema Joseph
Alisema kuwa Sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11ya mwaka
2007 imetamka kuwa kosa chini ya Kifungu Cha 25 " Mtu yeyote ambaye kwa
kutumia nafasi yake au Mamlaka yake katika kutekeleza majukumu yake
anadai au analazimisha upendeleo wa Kingono au upendeleo mwingine wowote
Kama kigezo Cha kutoa ajira , Kupandishwa cheo, Kutoa haki au
upendeleo wowote unaotambulika Kisheria atakuwa ametenda Kosa" ,alisema
Joseph.
Alisema kuwa kesi ya rushwa ya ngono zimekuwa zikishindwa mahakamani
kwa kukosa ushahidi uliojitosheleza kutokana na jamii kutokuwa na elimu
ya rushwa ya ngono.