Hii
itakuwa ni mara ya kwanza kwa chama hicho kushiriki maadhimisho hayo
yanayofanyika kila Desemba 9 tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwaka
2015.
Taarifa
iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema,
Tumain Makene imesema hatua hiyo inalenga kukuza na kuendeleza uraia
mwema, uzalendo na mapenzi ya nchi yetu.
“Kamati
kuu ya Chadema imeazimia kwa kauli moja kuwa Mwenyekiti wa Chadema,
Freeman Mbowe aongoze ujumbe wa baadhi ya viongozi wakuu na waandamizi
wa chama watakaokiwakilisha chama kushiriki katika maadhimisho hayo.”
“Chama
kinawaelekeza wanachama na wapenzi wake jijini Mwanza na maeneo ya
jirani kujumuika na Watanzania wengine kushiriki na kuadhimisha siku hii
muhimu kwa Taifa letu,” amesema Makene