RAIS MAGUFULI NA VIONGOZI WENGINE WA KISIASA WAOMBOLEZA KIFO CHA ALI MUFURUKI


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli  amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za  kifo cha Mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Ali Mufuruki, aliyefariki Dunia akiwa nchini Afrika ya Kusini.


Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Kijamii wa Twitter, leo Desemba 8, 2019, ameandika;  Nimehuzunishwa na taarifa za kifo cha rafiki yangu Ali Mufuruki (Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji wa Kampuni - CEOrt) Nitamkumbuka kwa uzalendo na mchango wake katika kukuza sekta ya biashara na ushauri kwa Serikali.Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.


Mbunge wa Kigoma Mjini, na kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameandika; "Sina maneno ya kusema zaidi ya kuwa sote ni wake Mwenyezi Mungu na kwake sote tutarejea, sio tu alikuwa rafiki bali alikuwa mshauri wangu, tulipishana mawazo fulani lakini alikuwa na heshima kubwa, tangulia ndugu yangu RIPMufuruki" 


Mwanasiasa mwingine aliyeonesha kuguswa na msiba wa Ali Mufuruki ni mwanasiasa wa muda mrefu Khamis Kagasheki, ambaye ameandika hivi; "Kwa mshtuko na masikitiko nimepata taarifa kwa kifo cha Ndg Ali Mufuruki, pigo kubwa kuondokewa na Ali, mkono wa pole nyingi kwa familia yake, MwenyeziMungu amhurumie na amsamehe. Ali you will be missed immensely".


Nape Nnauye yeye kaandika; Ni kazi ngumu sana kusimamia kile unachoamini hasa kama kitendo hicho kitakufanya msielewane na marafiki na watu wako wa karibu, LAKINI wewe Ally Mfuruki uliweza kuwa imara na mkweli kwa ulichoamini! Pumzika kwa amani!"


Kwa upande wake Maalim Seif yeye kaandika; "Nimepokea kwa huzuni, masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Ndugu Ali Mufuruki @amufuruki kilichotokea jana katika Hospitali ya Morningside, Johannesburg, nchini Afrika Kusini. Mwenyezi Mungu Amlaze mahala pema Peponi. Amin. Hakika sisi ni wa Mungu na Kwake Yeye Tutarejea."

Wengine walioguswa na kutuma salamu za pole kwa ndugu jamaa na marafiki wa mfanyabiashara huyo ni pamoja na Ubalozi wa Ujerumani hapa nchini Tanzania.
Ali Mfuruki aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Vodacom Tanzania, aliyehudumu kwa muda wa miaka miwili, ambapo baadaye alitangaza kujiuzulu nyadhifa zake zote

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post