Chama
cha Conservative kimeshinda zaidi ya viti 326 vya Ubunge huku Kiongozi
wa Chama hicho Boris Johnson akiwashukuru wapiga kura wa Uingereza kwa
kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi huo.
Waziri
Mkuu Boris Jonhson amesema ushindi huo unaipa Serikali mpya fursa ya
kuheshimu maamuzi ya kidemokrasia ya Raia wa Uingereza, Boris Johsnon na
Chama chake walihitaji kupata viti 326 ili kutangazwa kuwa Washindi
lakini wamepitisha idadi hiyo.
Huenda wingi huo wa kura za Wawakilishi Bungeni ukamuwezesha Borris
kuufanikisha mpango wake wa Brexit na kuiondoa Uingereza kwenye EU kabla
ya Mwezi wa pili Mwakani.
Ufaransa imesema ushindi wa Waziri Mkuu Boris Johnson utawezesha kutekelezwa mchakato wa Brexit kwa utaratibu mzuri.