Mkuu
wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, ameagiza kukamatwa kwa Kapteni
Mstaafu mkoani Kilimanjaro John Mushi, kwa madai ya kumiliki kwa mabavu
eneo la TANESCO kwa zaidi ya miaka 35, huku akiwa halipii kodi ya ardhi
anayodaiwa ambayo ni zaidi ya Milioni 20.
Eneo
hio lenye ukubwa wa mita za mraba 3,371 mali ya Shirika la Umeme
Tanzania (Tanesco) linadaiwa kumilikiwa na Mushi tangu mwaka 1984 huku
kodi ikilipwa na Tanesco. Anadaiwa hana nyaraka zozote zinazomruhusu
kufanya hivyo.
Sabaya pia ameagiza mali zilizokuwepo katika eneo hilo vikiwamo vifaa
vya ujenzi kuzuiwa na mashine ya kufyatua matofali kupelekwa katika eneo
la ofisi yake mpaka Mushi atakapolipa kodi ya miaka 35 aliyolipiwa na
Tanesco
Sabaya ametoa agizo hilo jana Jumatatu Desemba 2, 2019 baada ya
kutembelea eneo hilo, kutoa siku 30 kwa Tanesco kuhakikisha wanazungusha
ukuta eneo lote na siku 60 kuanza ujenzi wa jengo la kisasa.