Na Mwandishi Wetu Arusha
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu amewataka wananchi
kuhakikisha wanaboresha makazi yao kutoka makazi ya nyumba za nyasi na
tembe kwenda nyumba za tofali na bati.
Aliyasema
hayo leo Wilayani Monduli mkoani Arusha alipokuwa akitembelea miradi
mbalimbali ya maendeleo iliyoamasishwa na wataalam kutoka Chuo cha
Maendeleo ya Jamii Monduli kwa kuamsha ari ya wananchi kushiriki katika
miradi ya Maendeleo.
Dkt.
Jingu aliwataka wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini kuhakikisha
wanakuwa chachu ya mabadiliko na wanawezesha jamii kuwa na mawazo chanya
ya kujiletea maendeleo na kubadili changamoto kuwa fursa za
kimaendeleo.
"Wataalam
wa Maendeleo ya Jamii tuweke nguvu katika kuhakikisha tunabadili jamii
zetu kuwa na mawazo chanja hasa ya kujitegemea na kujiletea maendeleo"
alisema Dkt. Jingu.
Dkt.
Jingu aliongeza kuwa Sekta ya Maendeleo ya Jamii inapaswa kuwa chachu
ya maendeleo katika taifa letu hivyo Vyuo vya Maendeleo ya Jamii
vinatakiwa kutoa wataalam wenye weledi na stadi za kubwa za kuleta
mabadiliko katika jamii.
"Vyuo
vya Maendeleo ya Jamii tutoe wataalam wenye weledi wa kuhakikisha
tunatumia fursa zilizopo katika jamii kutatua changamoto zilizopo"
alisema Dkt. Jingu.
Wakati
huohuo akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli
Dkt. Jingu amewataka wanafunzi hao kusoma kwa bidii na kuhakikisha
wanatumia stadi watakazopata kubadilisha maisha yao na jamii kwa ujumla.
Dkt.
Jingu aliwataka wanafunzi hao kuitumia bahati ya kuwa mmoja ya
wanafunzi katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli kwa kuhakikisha
wanafanikisha ndoto zao walizozilenga kuzitimiza katika maisha yao kwa
kuzingatia masomo na nidhamu.
Kwa
upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Monduli Bw.
Elibariki Ulomi alimuhakikishia Katibu Mkuu kuwa Chuo hiyo kitahakikisha
kinashirikiana na wananchi wa Wilaya ya Monduli katika kutekeleza
Kampeni ya Makazi Bora ili kuwawezesha wananchi kuboresha makazi yao na
kuhakikisha kinatoa Wataalam wa Maendeelo ya Jamii watakosaidia kuleta
mabadiliko katika taifa.
Naye
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Monduli Bi. Rose Mhina alisema kuwa
Halmashauri hiyo imeshaanza kutekeleza kampeni ya Makazi bora kwa
kuipeleke ajenda hiyo kwa madiwani na kutoa michoro maalum kwaajili ya
ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu.
Aliongeza
kuwa Kampeni hiyo ya kuhamaisha ujenzi wamakazi bora itahamasishwa na
katika jamii na maafisa Maendeleo ya Jamii kutoka wilayani maoaka kwemye
kata ili kuhakikisha wananchi wanajitoa na kuboresha makazi yao.
Kampeni
ya Kuboresha makazi inalenga kuiwezesha jamii ambayo inaishi katika
makazi yasiyo bora kuweza kuboresha makazi yao kwa kutumia ramani
ziliziotolewa na Halmashauri walizopo zikiwa ni nyumba za gharama nafuu.