Liverpool waibuka mabingwa wa
kombe la Klabu Bingwa wa Dunia, baada ya kuifunga Flamengo ya nchini
Brazil bao 1:0 katika mchezo wa fainali.
Roberto Firmino alifunga bao pekee la Liverpool katika mechi hiyo ya fainali iliyopigwa mjini Doha Qatar.
Liverpool imekua timu ya pili
kutoka England kushinda ubingwa Wa Dunia kwa ngazi ya vilabu baada ya
Manchester United kufanya hivyo mwaka 2008.