Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw.
Gabriel Daqaro akianza ukaguzi wa mabanda ya wajasiliamali wanawake
kabla ya kufunga Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi jana Jijini
Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw.
Gabriel Daqaro akiangalia bidhaa aina ya mvinyo unaotengenezwa na Bi.
Magreth Ibrahim wa Joma Enterprises kabla ya kufunga Kongamano la
Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi jana Jijini Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw.
Gabriel Daqaro akianza ukaguzi wa mabanda ya wajasiliamali wanawake
kabla ya kufunga Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi jana Jijini
Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw.
Gabriel Daqaro akitoa ushauri kwa wajasiliamali wanawake wanaotengeneza
Nguo aina ya batiki wakati wa ukaguzi wa mabanda ya wajasiliamali
wanawake walioshiriki Kongamano la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi jana
Jijini Arusha.
………………
Na Mwandishi wetu APC BLOG, ARUSHA
Mkuu wa Wilaya ya
Arusha Bw. Gabriel Daqaro amewataka wanawake wajasiliamali Mkoani
Arusha kuwa wazalendo kwa kulipa kodi pale biashara yao inapokuwa
kubwa kwa kuwa jukumu la kujenga Nchi ni la kwetu sote akionya kuwa
baadhi ya watu wasidhani hawana jukumu la kujenga Nchi.
Pamoja na mambo
mengine Bw. Daqaro amewataka wanawake wajasiliamali hao kutumia fursa
waliyopata ya elimu ya ujasiliamali kuwasaidia kuwekeza ili waweze
kubadilisha maisha yao, familia na Taifa kwa ujumla.
Bw. Daqaro
Ameyasema hayo wakati wa hotuba yake yakufunga Kongamano la Siku mbili
la uwezeshaji wanawake kiuchumi waliokusanyika kutoka Wilaya za Mkoa wa
Arusha na kuongezewa ujuzi kwa kupatiwa mafunzo ya ujasiliamali.
Aidha Bw. Daqaro
amewataka Wajasiliamali hao kurasimisha biashara ili waweze kuwa katika
mfumo unaojulikana unaotambulika na serikali ili wote tushirikiane
kujenga Taifa letu na kuwataka kutambua kuwa inabidi kushirikiana na
serikali kujenga Nchi hii.
Bw. Daqaro
amewataka wajiasiliamali hao wanawake kuzingatia viwango vya ubora
katika bidhaa zao ili ziweze kushindana katika soko kwa kuhakikisha
wanakuwa na vifungashio imara na bora ili bidhaa zao ziweze kukidhi
ubora na kushindana katika soko.
Amelitaka Shirika
la Viwanda vidogo Nchini SIDO kuendelea kutoa elimu ya biashara kwa
vikundi vya akina mama ili viweze kuzalisha bidhaa bora zinazoweza
kushindana katika Soko.
Akiongea wakati
wa kufunga Kongamano hilo Bi. Mboni Mgaza Mkurugenzi Msaidizi sehemu ya
Wanawake kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii amesema
washiriki wa Kongamano la Uwezeshaji Wanawake kiuchumi walifikia 200 na
wamepatiwa mafunzo mbalimbali ua ujasiliamali pamoja na uzalishaji
bidhaa kwa lengo la kukuza uwezo wao wa kiuchumi.
Bi. Mboni Mgaza
pia wanawake kupitia Kongamano hilo wameweza kuonesha na kuuza bidhaa
zao lakini pia kuna baadhi ya wanawake ambao wamepatiwa mafunzo na
Taasisi mbalimbali ambazo zilitoa jumla ya mada 13.
Naye Mshiriki wa
Kongamano hilo Bi. Irene Paranjo amesema Kongamano hilo limeleta faida
kwa wanawake hao kwani wameweza kujenga mtandao lakini pia kubadilishana
Mawazo ya namna ya kuboresha biashara zao lakini pia imekuwa ni fursa
kwao kukutana na viongozi wa juu ambao wamehaidi kuwasaidia katika
juhudi za Serikali za kuwezesha wanawake kiuchumi.
Serikali imekuwa
ikitoa Mikopo kupitia Serikali za Mitaa kwa Wanawake waliokatika vikundi
vya hisa na ujasiliamali kwa lengo kuwezesha wanawake kiuchumi na
tayari Serikali tayari kupitia mapato ya Halmashauri zote Ncini inatenga
asilimia kumi ya mapato yake kwa lengo la kuwezesha wanawake vijana na
walemavu.