Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akisisitiza
jambo kwa Mbunge wa Mbogwe mhe, Augustino Masele alipokagua utekelezaji
wa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe
Joseph Magufuli la kuutaka Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA),
wilayani Mbogwe kujenga kilometa 3 za barabara za lami katika makao
makuu ya wilaya hiyo kulia ni mkuu wa wilaya hiyo Bi. Martha John
Mkupasi.
Meneja wa (TARURA), wilayani
Mbogwe mkoani Geita Eng. Justine Lukaga, akisisitiza jambo kwa Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius
John Kwandikwa alipokagua barabara ya Mang’ombe-Iloganzala Km 1.2,
ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umeanza katika mji wa Masumbwe
Wilayani humo.
Muonekano wa barabara ya
Mang’ombe-Iloganzala Km 1.2, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami
umeanza katika mji wa Masumbwe Wilayani Mbogwe Mkoani Geita.
Mkuu wa wilaya ya Mbogwe mkoani
Geita Bi, Martha John Mkupasi (wapili kushoto), akisisitiza jambo kwa
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe.
Elius John Kwandikwa alipokagua barabara zinazojengwa na TARURA kwa
kiwango cha lami wilayani humo.
Kazi ya usafishaji wa barabara ya
Mang’ombe – Iloganzala Km 1.2, inayojengwa kwa kiwango cha lami
wilayani Mbogwe mkoani Geita ikiendelea ikiwa ni utekelezaji wa agizo la
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli
kuwataka TARURA kujenga barabara za lami zenye urefu wa km 3 wilayani
humo.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa akifafanua
jambo kwa waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli wa
kuwataka TARURA kujenga barabara za lami zenye urefu wa Km 3 wilayani
Mbogwe.
Na Mwandishi wetu, Mbogwe
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), mhe. Elius John Kwandikwa amewataka
viongozi wote wa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kushirikiana na Wakala wa
Barabara Vijijini (TARURA), kuhakikisha ujenzi wa barabara za lami
katika mji wa Masumbwe unakamilika kwa wakati.
Amesema uwepo wa barabara nyingi
za lami katika wilaya za Mbogwe na Kahama utachochea fursa nyingi za
utalii, ufugaji, uchimbaji madini na uzalishaji wa mazao ya chakula na
biashara na hivyo kukuza uchumi wa jamii na taifa kwa ujumla.
Akizungumza mara baada ya kukagua
ujenzi wa barabara zinazosimamiwa na TARURA wilayani humo mhe. Kwandikwa
amesema atahakikisha ujenzi wa kilomita zote tatu zilizoahidiwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Joseph Magufuli
unakamilika kama ilivyopangwa.
“Hakikisheni mnawaelimisha
wananchi ili wapishe maeneo yote zitakapopita barabara hizo ili kusiwe
na vikwazo kwa wajenzi wa barabara hizo”, amesisitiza Naibu Waziri
Kwandikwa.
Hivi karibuni katika ziara yake
wilayani humo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe
Joseph Magufuli aliagiza utekelezwaji wa haraka wa ujenzi wa barabara
zenye urefu wa kilometa tatu alizoahidi katika makao makuu ya wilaya ya
Mbogwe na kusisitiza kazi hiyo ifanyike haraka.
Naye mkuu wa wilaya ya Mbogwe Bi,
Martha John Mkupasi amesisitiza umuhimu wa wananchi kutoa ushirikiano
wakati wa ujenzi wa barabara hizo na kuzilinda pindi zitakapokamilika
ili kuboresha miundombinu ya wilaya hiyo na kukuza shughuli za biashara.
Amehimiza wananchi kutovamia maeneo ya hifadhi ya barabara ili kuepuka usumbufu wakati zoezi la ujenzi linapoendelea.
Kwa upande wake meneja wa TARURA
wilayani humo Eng. Justine Lukanga ameahidi ujenzi wa kilometa tatu za
lami katika barabara ya Mashineni-Kasandalala km 1.3 na
Mang’ombe-Iloganzala 1.2 na kituo cha afya-shuleni km 0.5 zitajengwa kwa
kasi na ubora unaozingatia thamani ya fedha.