Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP
Mtandao) umeendesha warsha ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa
habari wa mikoa mbalimbali nchini waliopewa mafunzo juu ya ushiriki wa
wanawake katika uongozi ikiwemo siasa.
Warsha hiyo ya siku mbili imeanza leo Jumanne Desemba 17,2019 kwenye
ukumbi wa mikutano wa Silver Paradise Hotel jijini Dar es salaam.
Warsha hiyo imekutanisha waandishi wa habari kutoka mikoa ya
Shinyanga,Rukwa,Kilimanjaro, Ruvuma,Pwani,Morogoro na Dar es salaam kwa
ajili ya kuwajengea na kuongezea uelewa na uwezo wa kuripoti masuala ya
kijinsia hasa katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake na vijana kwenye
uongozi.
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John amesema lengo ni kuvuna matokeo
yaliyotokana na mafunzo yaliyofanyika mwezi Septemba mwaka huu juu ya
ushiriki wanawake katika uongozi.
“Kupitia warsha hii washiriki wataelimishwa juu ya ilani ya uchaguzi
ya wanawake na kuweka mikakati ya namna ya kuongeza kasi ya kuripoti
masuala ya kijinsia kwenye vyombo vya habari hasa kusambaza ilani ya
uchaguzi ya wanawake na kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki
wa wanawake na vijana katika uongozi”,ameeleza John.
“Tutajadili changamoto,mafunzo na fursa zilizopo katika vyombo vya
habari katika kuhamasisha jamii kuchagua na kuhamasisha wanawake
kushiriki katika uongozi”,amesema John.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza wakati wa warsha
ya kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari wa mikoa mbalimbali
nchini waliopewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi
ikiwemo siasa leo Jumanne Desemba 17,2019 katika ukumbi wa Silver
Paradise Hotel jijini Dar es salaam. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John ambaye ni Mwezeshaji katika
warsha hiyo akieleza namna waandishi wa habari wanavyoweza kutumia
kalamu zao kuhamasisha mila nzuri zinazohamasisha ushiriki wa wanawake
na vijana katika uongozi.
Afisa Habari wa TGNP Mtandao Monica John akizungumza kwenye warsha ya
kuvuna matokeo kutoka kwa waandishi wa habari wa mikoa mbalimbali nchini
waliopewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo
siasa.
Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa ukumbini.
Waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania wakiwa ukumbini.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Nipashe Marco Maduhu kutoka mkoa wa
Shinyanga akitoa mrejesho wa kazi alizofanya baada ya kupewa mafunzo juu
ya ushiriki wa wanawake katika uongozi ikiwemo siasa.
Mwandishi wa habari Bahati Nyakiraia kutoka mkoa wa Kilimanjaro akitoa
mrejesho wa kazi alizofanya baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa
wanawake katika uongozi ikiwemo siasa.
Mackline Kamote wa Abood Media Morogoro akitoa mrejesho wa kazi
alizofanya baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika
uongozi ikiwemo siasa.
Angel Mbalamwezi wa Nkasi Fm Rukwa akitoa mrejesho wa kazi alizofanya
baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi
ikiwemo siasa.
Rodrick Mushi wa Star Tv mkoani Kilimanjaro akitoa mrejesho wa kazi
alizofanya baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika
uongozi ikiwemo siasa.
Aden Mbelle wa Jogoo Fm mkoani Ruvuma akitoa mrejesho wa kazi alizofanya
baada ya kupewa mafunzo juu ya ushiriki wa wanawake katika uongozi
ikiwemo siasa.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Washiriki wa warsha wakiwa ukumbini.
Warsha inaendelea.
Warsha inaendelea.
Washiriki wa wasrha wakiwa katika kazi ya kundi.
Kazi ya kundi ikiendelea.
Kazi ya kundi ikiendelea.
Washiriki wa warsha wakijadili jambo ukumbini.