Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, ametangaza
kuwaachia wafungwa 5533 ambao walikuwa wamefungwa katika Magereza
mbalimbali nchini.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho wa miaka 58 ya
Uhuru wa Tanzania Bara, ambapo kuna idadi kubwa ya wafungwa ambao wapo
Magerezani kwa makosa ya kawaida sana.
“Nilitembelea
Magereza nikashuhudia kuna mlundikano wa wafungwa, mpaka leo kuna
Wafungwa 17,547 na Mahabusu 18,256, hii ni idadi kubwa, kwa hao wafungwa
kuna baadhi wamefungwa makosa madogo, sijui kaiba kuku, kujibizana na
mpenzi wake.
“Leo natangaza kuwasamehe wafungwa 5,533, ni mara ya kwanza kwa msamaha
mkubwa kama huu kutokea, najua watu watashangaa lakini nimetumia siku
hii ya Uhuru kusamehe, sifurahi kuongoza nchi yenye watu wengi
Magerezani.
“Msamaha huu utawahusisha wafungwa waliofungwa kati ya kipindi cha siku
moja hadi mwaka mmoja, na wale Wafungwa waliofungwa Miaka mingi kama 30,
20, 10 au mitano na wamebakiza muda mfupi kumaliza. Aliyewasamehe ni
Mungu.” Rais Magufuli.