Serikali imesema
inapanga kununua ndege ya mizigo itakayosafirisha shehena ya bidhaa za
maua na mbogamboga kwa lengo la kuongeza fursa za uwekezaji na biashara
kwa wakulima nchini.
Mapango
huo unaokusudia kuongeza na kuimarisha sekta ya usafirishaji kwa njia
ya anga ndani na nje ya Tanzania utawezesha safari za moja kwa moja za
bidhaa hizo kwenda na kutoka nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na Rais Magufuli jana Jumamosi katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza wakati wa shughuli ya mapokezi ya ndege aina ya Bombardier Q-400
Alisema
mikakati hiyo ndiyo maana Serikali inajenga vyumba vya barafu vya
kuhifadhi maua na mbogamboga katika uwanja wa Mwanza, Songwe na Mbeya.