TANESCO IPO TAYARI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI

NA FARIDA SAIDY,MOROGORO 

Shirika la umeme Tanzania TANESCO limesema lipo tayari  kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Pombe Mafuli,ya kuleta maendeleo kwa wananchi, ambapo kwa mala ya kwanza shirika hilo limetoa gawio kwa serikali la shilingi bilioni 1.436.

Akizungumza wakati akifunga mkutano wa baraza kuu la 49 la wafanyakazi wa tanesco mkoani Morogoro Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanesco Dkt Alexander Kyaruzi alisema kuwa huo ni mwanzo mnzuri kwa shirika  katika kuleta maendeleo ya taifa,ambapo serikali inamiliki hisa za shirika hilo asilimia mia moja.

Katika hatua nyingine aliwataka wasimamizi wanaosimamia miradi  ya kusafirisha umeme wa msongo wa kilovati 400 wa Singida –Arusha hadi Namanga ,na ule wa iringa –mbeya  hadi Tunduma kuharakisha miladi hiyo ili kufanikisha adhima ya serikali ya awamu ya tano ya kuunganisha mifumo miwili ya gridi ya taifa ya nchi za kusini mwa afrika(SOUTHERN AFRICA POWER POOL-SAPP)  na ule wa nchi za afrika mashariki (EASTERN AFRICA POWER POOL-EAPP)inafanikiwa.

 Aidha aliongeza kuwa kukamilika kwa miladi hiyo ya kusafirisha umeme wa kilovati 400 na ule wa kuzalisha umeme wa Julius nyerere (JULIUS NYERERE HYDROPOWER PROJECT –JNHPP)utaifanya Tanzania kuwa kati ya nchi zinazouza  umeme kwa mataifa mengine .

Sambamba na hayo  Dkt Kyaruzi amewataka wafanyakazi wa Tanesco kuwa makini pindi wawapo katika majukumu yao ya kazi,hususani wanapokuwa safarini kwa kuhakikisha madereva wa shirika hilo wanafuata sheria za usalama barabarani,haswa katika swala zima la spidi wawapo safarini

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post