Washiliki wa Mafunzo ya Shindano la Usalama wa mitandao kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu. |
Mkurugenzi wa Tehama wa TCRA Connie Francis akiwa na washiliki wasichana wa Shindano la Usalama wa mitandao Vyuo vikuu |
Mkuu wa Kanda ya Kati wa TCRA Antonio Manyanda akizungumza kuhusiana na utaratibu uliotumika kupata washiriki wa Shindano la Usalama wa mitandao kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu lililifungwa mjini Dodoma. |
Mshauri wa Maendeleo ya Biashara wa Silensec wa nchini Kenya Kapere Ndege akitoa mafunzo kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu walioshiriki Shindano la Usalama wa Mitandao. |
*TCRA yawapongeza Wanafunzi wa walioshiriki Shindano la Usalama wa mitandao
Na Mwandishi Wetu
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) ni Teknolojia ambayo inabadilika kila siku hivyo kunahitaji mafunzo katika usalama wa mitandao.
Hayo ameyasema Mwakilishi wa Wizara ya Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Richard Mgema wakati kufunga Shindano la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini la Usalama wa Mitandao lililoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa Kushirikiana na Kampuni ya Nchini Kenya lilofanyika Jijini Dodoma.
Mgema amesema kuwa Dunia iko katika mabadiliko ya Tehama kila siku ambapo Tanzania hatuwezi kuwa kisiwa cha kutoendana na Teknolojia hiyo.
Amesema Wanafunzi walioshiriki Shindano hilo wamekwenda katika mchujo mbalimbali hivyo washindi watakwenda kushindana na nchi nyingine katika suala la ulinzi katika mitandao.
Aidha amesema kuwa kama nchi kumekuwa na mabadiliko ya huduma za fedha kwenda katika mitandao hivyo vijana wengi wanahitajika kuhusiana na kujua mifumo ya ulinzi wa mitandao ili Fedha za Wananchi ziwe salama.
Amesema Tehama ukuaji wake ni kasi kutokana na mifumo ya kiteknolojia kubuniwa hivyo lazima kuwapo kwa Rasilmali Watu ya kwenda kwa kasi katika Teknolojia hizo.
Nae Mkuu wa Kanda ya Kati wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Antonio Manyanda amesema kuwa wakati wa usajili wa Shindano la Usalama wa Mitandao Wanafunzi wa Vyuo Vikuu walikuwa 1056 baada ya mchujo wa Kwanza walipatikana Wanafunzi 600 na mchujo wa Tatu walipatikana Wanafunzi 50 katika Vyuo Vikuu Nane.
Manyanda amesema kuwa Wanafunzi hao waliokuwa wanashiriki Shindano hilo walikuwa ni wale wanaosoma Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT) na umri wao kati ya Miaka 18 hadi 24.
Amesema walioshiriki wote ni washindi kwani wamepita katika Makundi mbalimbali hadi kufika hatua ya mwisho ya kupatikana kwa washindi wawili.
Mkurugenzi wa Tehama wa TCRA Connie Francis amesema kuwa katika Shindano hilo amegundua wasichana hawako nyuma kwani wanashiriki Shindano hilo.
Amesema kuwa dunia haijabagua wanawake kuwa kuna vitu vya kufanya wanaume tu.
Amesema walioshiriki waendelee kusoma kwa bidii kwa kuleta mabadiliko katika Tehama kwa dunia ndio iliko huko.
Washindi wa Shindano hilo wa Kwanza ni Godwin Mpapalika na Mshindi wa Pili Karim Muya.