Na Ahmed
Mahmoud Mererani
Wanafunzi zaidi
ya 400 wapo hatarini kutokujiunga na masomo ya kidato cha kwanza mwakani kutokana
na ukosefu wa vyumba vya madarasa unaozikabili shule mbili za Sekondari Benjamini Mkapa na Tanzanite zilizopo katika mji
mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Kwa Muktadha huo Ofisi ya
madini imewataka Wachimbaji,madalali na wafanyabiashara wa madini kuahakikisha
wanarudisha kile wanachovuna kwa kuchangia maendeleo ya jamii kwa ajili ya
ujenzi wa madarasa 10 ya wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza mwakani.
margin-right: 0in; text-align: justify;"> Akizungumza katika kikao cha wachimbaji,Madalali na wafanyabiashara Jana Afisa madini Mererani,Daud Ntalimwa alisema sheria ya mwaka 2017 kifungu 105 na 106 kinawataka wafanyabiashara,madalali na wachimbaji kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo shule ili kupunguza idadi ya wanafunzi kukosa madarasa na madawati.
Alisema kuwa
jumla ya million 200 zinahitaji kufanikisha ujenzi huo wa madarasa ili
wanafunzi mia nne wapate nafasi ya kujiunga na kidato cha kwanza mwakani
tunatoa siku 20 kuanzia leo Dec.2.
"Mchango
huu utabadilisha mtazamo wetu kuwa eneo letu ni la watu wakorofi na serikali
kuona ni wadau muhimu sana kwa siku za usoni itakuwa nchi imeshawatambua na hii
itakuwa mara ya kwanza kuchangia na kurudisha kwa jamii kile mnachipata kwa
mujibu wa sheria" alisema Ntalimwa.
Alisema kuwa
fedha hizo wanazochanga zitaisadia jamii bila kujali chochote hivyo wajibu wao
ni kujitoa kwa moyo mkubwa kuweza kufanikiwa ili jamii iliyowazunguka ipate
mafanikio kwa kile wanachovuna.
Alieleza kuwa
jumla ya fedha zitakazopatikana baada ya kuchangisha ni takribani milion 161
ikiwa wafadhili 400 watoa takribani million 1 ambapo madalali 410 watatoa
100,000 kila moja wachimbaji 50 watoa 500,000 kila kampuni.
Awali
akiongea Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii halmashauri ya wilaya ya
Simanjiro, Kilempu Laizer alisema kutokana na ufaulu wa watoto 700 wa Merelani
kuongezeka kwa mwaka huu hivyo na upungufu wa madarasa hupo kwa shule hizo
hivyo tukaomba wananchi na wadau wa madini tushirikiane kujenga madarasa na
madawati ili watoto wasiteseke kwa kukaa chini.
"Watoto
wa merelani wanateseka sana kuhusu swala la elimu hivyo tukaomba kila mtu
na nafasi yake anastahili kuchangia kwani ni aibu sana ikiwa baadhi ya
wanafunzi 300 watapelekwa shule ya sekondari Benjamin Mkapa na Songambele huku
400 watakosa madawati," alisema Mwenyekiti huyo.
Hata hivyo
wadau wa madini Mererani Dkt.Jacob Shegga mkurugenzi wa Covenant Ltd na Kilia
Laizer wamesema kuwa suala kulipia huduma za jamii ni jambo ambalo hawalipingi
na limekuja wakati muafaka ila utaratibu uboreshwe na uwe endelevu ili kuweza
kuboresha kijiji chetu.
Walisema kuwa
mkanganyiko wanaoupata umetokana na akaunti kuchanganywa na kuomba mji mdogo
uwe na akaunti ya malipo ya huduma za jamii pekee ili kuwaondolea suala hilo la
mkanganyiko huo.