WAZIRI MWAKYEMBE AMPONGEZA WALLACE KARIA KWA KUCHAGULIWA KUWA RAIS WA CECAFA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe ametoa pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Wallace Karia kwa kuchaguliwa kuwa Rais  wa Baraza la Soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA. 


Dkt. Mwakyembe amesema kuwa wizara itaendelea kushirikiana na  Bw.Karia ili kuhakikisha mafanikio ya CECAFA yanafikiwa katika kipindi cha uongozi wake pamoja na kuendeleza soka la hapa nchini. 


Bw. Karia anachukua nafasi ya Mutasim Gaffar wa Sudan aliyemaliza muda wake na ataongoza shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne kuanzia sasa, huku akiwa  Mtanzania wa pili kushika wadhifa huo  baada  ya Bw.Leodger Tenga. 

Aidha,  nafasi ya  Makamu wa Kwanza wa Rais imechukuliwa na Francis Amin wa Sudan Kusini na nafasi ya Makamu wa Pili  Rais imechukuliwa na Jira Isayaa kutoka Ethiopia. Imetolewa na,                                                                        

Anitha Jonas
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post