Mshambuliaji
wa klabu ya Aston villa na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars',
Mbwana Samatta ameeleza masikitiko yake kufuatia maoni yasiyoridhisha ya
Watanzania katika mitandaao ya kijamii.
Samatta
amesema hayo kufuatia Watanzania kutoa maoni yasiyoridhisha yakiwemo
matusi katika kurasa za klabu ya Aston Villa na kurasa za wachezaji wa
timu hiyo, wakidai kuwa mchezaji wao hapewi nafasi nyingi uwanjani.
Kupitia
ukurasa wake wa Twitter, Samatta ameandika, "mashabiki wa soka Tanzania
nafahamu kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vizuri katika
timu yangu mpya, lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye
mlengo mbaya katika kurasa za timu au wachezaji, binafsi sifurahishwi".