SAADAN YATUMIA BILIONI 1.1 KUSAIDIA MIRADI YA KIJAMII

Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae akizungumza na waandishi wa habari 
Afisa Uhifadhi wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Prisca Lyimo akielezea mikakati waliokuwa nayo
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Martina Ngulei akizungumza kuhusu namna walivyonufaika na uwepo wa hifadhi hiyo
Afisa Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Saadan Athuman Mbae katikati akiwa na wageni kutoka mataifa mbalimbali waliotembelea hifadhi hiyo
Sehemu ya wageni wakifurahia utalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadan
Aina ya malazi yanayopatikana kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadan kwa wageni wanaofika kutembelea vivutio mbalimbali
Mamba akiwa pembezoni mto Wami akiota jua kama alivyokutwa ambapo jamii ya Mamba wanapatikana pia kwenye hifadhi hiyo
Wanyama aina ya Viboko wakiwa kwenye maji ndani ya Mto Wami ambao umepita kwenye hifadhi hiyo ya Taifa ya Saadan kama wanavyoonekana
 Kundi la Wanyama aina ya Swala wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan

 Wanyama aina ya Pundamilia wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Aina ya Makundi ya Ndege ambayo yamejenga kiota kwenye hifadhi ya Taifa ya Saadan ndani ya Mto Wami ambapo ndege hao huishi pamoja ambao huishi hapo kwa ajili ya kuijepusha na maadui zao
 Wanyama aina ya Pundamilia wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Wanyama aina ya Twiga wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Wanyama aina ya Ngiri wakila majani ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Mnyama Ngiri akiwa anakula majani karibu na bahari ya hindi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Ndege aina ya Fundi Chuma akiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Saadan
 Mtalii akifurahia upepo wa bahari ndani ya Taifa ya Saadan


Hifadhi ya Taifa ya Saadani imetumia kiasi zaidi ya sh Bil 1.1 kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwenye vijiji 11 Kati ya 16 vinavyozunguka hifadhi hiyo kupitia mpango wa ujirani mwema.


Hayo yalisemwa na Afisa utalii wa hifadhi hiyo Athuman Mbae wakati akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea hifadhi hiyo hivi karibuni kujionea shughuli za utalii.


Alisema kuwa jumla ya miradi 23 iliyoko kwenye sekta za Afya, Elimu, Maji na Mazingira imeweza kufadhiliwa na hifadhi hiyo kwa kushirikiana na wananchi.


"Tumekuwa tukishiriki katika miradi ya ujirani mwema ambapo hifadhi inachangia asilimia 90% huku wananchi wakichangia asilimia 10% kwa lengo la kuhakikisha wanaweza kuituza miradi hiyo"alisema Mbae.

Awali akizungumza Afisa Uhifadhi wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Saadan Prisca Lyimo alisema kwamba alisema maboresho yaliyofanywa kwenye hifadhi hiyo na serikali ya awamu ya tano yamesaidia kuongeza idadi ya watalii wan je na ndani.

Alisema maboresho hayo yameongeza mwitikio wa watanzania kutembelea hifadhi za taifa kutokana na kuboresha miundombinu ufikaje wake huku watalii wanaweza kufika wakiwemo wa Zanznzar, Dar na Tanga na maeneo mengine hapa nchini.

“Bado tunaendelea kuhamasisha watanzania waone umuhimu wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo hapa nchini hususani hifadhi ya Kipekee ya Saadani inayopakana na Bahari ya Hindi”Alisema
 

Kwa upande wake Mtendaji wa Kijiji cha Saadani Martina Ngulei alisema kuwa hifadhi hiyo imeweza kusaidiana na wananchi katika kutatua kero mbalimbali ambazo zilikuwa zinatukabili.


"Hifadhi imeweza kutujengea nyumba ya Mwalimu,kusambaza maji kwenye nyumba za ibada sambamba na ujenzi wa choo chashule ambacho kilikuwa hakitumiki kwa muda mrefu kutokana na uchakavu"alisema Ngulei.


Nao baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Saadani wamesema kuwa kuishi kwa jirani na hifadhi kumekuwa ni neema kubwa kwao kwa kipato sambamba na fursa za biashara.


"Watalii wengine wakija wanaishi nje ya hifadhi hivyo tunapata kipato kwa kuwauzia chakula ikiwemo na malazi sambamba na kujifunza tamaduni za kwetu "alisemaAthuman Said.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post