Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, kulia ni Rais Mstaafu Daniel Moi wakati wa uhai wake.
Mwili wa aliyekuwa Rais wa Pili wa Jamhuri ya Kenya, Daniel Arap Moi,
tayari umekwishapelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kinachoitwa
Cha Lee, kilichopo jijini Nairobi nchini Kenya.
Rais Mstaafu wa Taifa hilo amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Februari
4, 2020, akiwa na umri wa miaka 95, katika hospitali Jijini Nairobi
alikokuwa akipatiwa matibabu na kifo chake kimetangazwa na Rais Uhuru
Kenyatta, akiwa safarini kuelekea nchini Marekani katika mkutano wake na
Rais Donald Trump.
Kufuatia kifo hicho Rais Kenyatta ametangaza kuwa bendera nchini Kenya
na katika Ubalozi wa Kenya, kupeperushwa nusu mlingoti hadi
atakapozikwa, ambapo hadi sasa taarifa za mazishi bado hazijatangazwa na
huenda Rais Kenyatta akasubiriwa, kwani atarejea nchini siku ya
Alhamisi ya Februari 6, 2020.
Daniel Moi aliingia madarakani mwaka 1978, baada ya kifo cha aliyekuwa
Rais wa kwanza Hayati Jomo Kenyatta, na kuapishwa kama Rais wa Pili wa
Jamhuri ya Kenya na kuhudumu kwa miaka 24, ambapo mkewe Lena Moi,
alifariki mwaka 2004.
Moi ameacha watoto Saba ambao ni Gideon (Seneta Baringo), Raymond
(Mbunge wa Rongai ), Jeniffer Moi, June Moi, Philip Moi, John-Mark and
Doris Moi. Mungu ailaze Roho ya Marehemu Daniel Arap Moi, mahala pema
peponi Ameen.