Jeshi
la polisi mkoa wa Kilimanjaro limemwachia Mchungaji Boniface Mwamposa
pamoja na wenzake saba(7) kwa dhamana baada ya kuridhishwa na maelezo
yao.
Akizungumza
leo katika Mkoa huo Msemaji wa jeshi la Polisi SACP-Misime amesema kuwa
kama ilivyokwisha kuelezwa na viongozi mbalimbali na kwenye taarifa
yake ya tarehe 03.02.2020 hatua mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa ni
kwamba baada ya tukio hilo Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon
Nyakoro Sirro (IGP) alituma timu ya maofisa wakiwepo wataalamu wa
Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai kwenda kuungana na timu ya wataalamu kule
Kilimanjaro katika uchunguzi.
“Katika
uchunguzi huo walikamatwa watu nane (8) akiwepo Bonifase Mwamposa na
kuhojiwa kwa kina na baada ya kujiridhisha na yale yaliyokuwa
yanahitajika kutoka kwao wamepewa dhamana kwa mujibu wa sheria ili
waendelee kuripoti wakati uchunguzi ukiendelea.
"Uchunguzi
bado unaendelea na baada ya kukamailika yatakayobainika yatatolewa kwa
mamlaka husika na kutelekezwa kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu.
"Hivyo kila mmoja anatakiwa awe na subira na uchunguzi unaofanywa na wataalam utakapokamilika mtajulishwa”. Amesema SACP-Misime.
"Hivyo kila mmoja anatakiwa awe na subira na uchunguzi unaofanywa na wataalam utakapokamilika mtajulishwa”. Amesema SACP-Misime.