Akitoa
taarifa hiyo mbele ya wanahabari, Mkurugenzi wa Opresheni wa NACTE, Dr
Geofrey Oleke amesema lengo la kuvifutia vyuo hivyo usajili ni kutaka
vikamilishe taratibu ili kutoa elimu yenye manufaa kwa Watanzania kwa
kufuata misingi.
Orodha
ya vyuo vilivyofutiwa usajili ni pamoja na ERA Training College -
Bukoba (REG/TLF/095), Azania College of Management - Dar es Salaam
(REG/BMG/021), Time School of Journalism - Dar es Salaam (REG/PWF/013),
Clever College - Dar es Salaam (REG/BTP/205P) na Aces College of
Economic Science - Mwanakwerekwe, Zanzibar (REG/BPT/081P).