Na.Vero Ignatus,Arusha
Jamii
imetakiwa kuondoka na na dhana potofu ya kumkeketa mtoto wa kike na
kumuondolea hadhi na utu wake kama Mungu alivyomuumba badala yake
wabadilike na kukemea kitendo hicho kwani ni ukiukaji wa haki za
kibinadamu
Ukeketaji
unawaathiri wasichana na wanawake kwa asilimia kubwa pia kitendo hicho
kinadhoofisha uchumi pamoja na nguvu kazi, unaathiri afya ya mwili na
akili za kwa wanawake wanaokeketwa hivyo jamii inapaswa kuungana ili
kupinga kitendo hicho
Hayo yamesemwa na Muwakilishi wa dini ya Wahabai mkoani Arusha John Msabi kwamba
mtu yeyote aliyepo karibia na jamii awe muhamasishaji wa kupinga mila
hizo mbaya na potefu zinazomkosesha ujasiri mtoto wa kike na mwanamke
Msabi amesema
mara nyingi watoto wa kike na wanawake hufanyiwa tunyanyasaji huo kwa
lazima na kwa maumivu makubwa, amekemea baadhi ya makabili yanayoamini
kuwa mwanamke asiyetahiriwa hawezi kuolewa jambo ambalo halina ukweli
wowote
Ikumbukwe
kuwa unapomkeketa mtoto wa kike unamsababishia maumivu makali,kutokwa
na damu nyingi wakati wa kujifungua kwani kovu lililopo halitanuki
hivyo humsababishia maumivu makali na hata wakati mwingine hupelekea
kupoteza Maisha yake pamoja na mtoto
Hivyo
basi Kila mwanajamiii anapaswa kushiriki kampeni kuhamasisha na kupiga
vita suala la ukeketaji kwa watoto wa kike na wanawake kwa ujumla
Ameitaka
jamii kutambua kuwa mtoto wa kike ni tunu hivyo unapomuelimisha
mwanamke umeielimisha jamii nzima kwasababu muda mwingi ndiyo wanakuwa
na watoto familia kwa asilimia kubwa kwa muda mrefu
‘’Kama
wewe ni mwalimu ,mchungaji ,shekhe kiongozi wa serikali kuanzia ngazi
zi za mtaa hadi Taifa siasasa wakati unaendelea na taratibu za kufanya
majukumu yako ya kila siku hakikisha umegusia suala hili la kupinga
ukeketaji kwa Watoto wakike na wanawake’’
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Arusha Yasmini Bachu amewataka
mamgariba ambao bado wanaendeleza tabia hiyo kuacha mara moja sambamba
na kuwaonya waache wanawakeketa watoto wachanga
'Bachu
amesema kuwa baada ya kuona serikali inakemea kitendo cha ukeketaji kwa
nguvu zote,mangariba wamebuni mbinu ya kuwakeketa watoto wachanga
kuanzia mwezi mmoja hadi miwili jambo ambalo ni hatari sana
‘'Tuwalaani
mangariba wote am,bao wanafanya kazi hiyo ya kuwakeketa Watoto wachanga
jambo hili ni baya sana na sisi hatutanyamaza bali tutapaza sauti
kukemea suala hili’alisema
Alisema
ndoa changa zinakuwa na migongano na kuvunjika kutokana,kuwa na
migogoro mingi isiyokwisha ila sehemu kubwa chanzo chake unakuta
mwanamke amekeketwa
Amesema
kuwa ukeketaji husababisha matatizo ya kiungo pamoja na yale ya kiakili
kwa mwanamke katika kipindi chote cha Maisha yake kilichosalia
kwasababu huathirika kisaikolojia siku zote
Kwa
mujibu wa shirika la Afya duniani (WHO) limesema kuwa ukeketaji
unaathiri wasichana na wanawake na gharama ya matibabu ni dola bilioni
1.4 kwa mwaka kimataifa iwapo mahitaji yote ya kiafya yatashughulikiwa.
Siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji hufanyika kila mwaka februari sita