UFARANSA YAONGEZA MWEZI MMOJA WA TAHADHARI DHIDI YA CORONA


Ufaransa imeongeza muda wa kuendelea kuchukua tahadhari za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona hadi Mei 11. 


Rais Emmanuel Macron amesema ifikapo tarehe hiyo shule zitaanza kufunguliwa. 

Jumatatu Ufaransa imeripoti vifo 574 vinavyotokana na maambukizi ya virusi hivyo, na kuifanya idadi jumla ya vifo kufikia watu15,000. 

Hata hivyo, idadi ya wagonjwa wa COVID-19 wanaohitaji uangalizi maalumu imepungua kwa siku ya tano mfululizo. 

Macron amesema kasi ya janga hilo inaanza kupungua na dalili za kudhihirisha hilo ziko wazi. “Mei 11 itakuwa mwanzo wa awamu mpya. Sheria zinaweza kubadilishwa kulingana na hali itakavyokuwa,” aliongeza Macron.

Serikali mbalimbali kote ulimwenguni ziko chini ya shinikizo la kuokoa uchumi wa dunia usije kuanguka kabisa kwa sababu ya kufungwa kwa biashara na watu kulazimika kubakia majumbani, lakini viongozi pia wanajaribu kuzuia wimbi la pili la ugonjwa huo.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post