Virusi vya corona: Idadi ya wagonjwa Tanzania yafika 147 baada ya wagonjwa 53 zaidi kukutwa na virusi hivyo

Kijana aliyevalia barakoaHaki miliki ya picha Getty Images
Tanzania imethibitisha visa vipya 53 vya ugonjwa wa corona nchini humo hatua inayoongeza idadi ya watu walioathirika na ugonjwa huo kufikia watu 147.
Katika taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari , waziri wa Afya Ummi Mwalimu amesema kwamba wagonjwa wote ni raia wa Tanzania.
Idadi hiyo ni kubwa zaidi kutangazwa kwa siku moja katika taifa la Afrika mashariki tangu wagonjwa wa kwanza wa virusi hivyo kugunduliwa katika eneo hili.
Amesema kwamba miongoni mwa wagonjwa hao 38 wanatoka katika mkoa wa Dar es salaam, 10 katika Kisiwa cha Zanzibar , mmoja kutoka Kilimanjaro , 1 kutoka Mwanza , Pwani Mtu 1 na Kagera mtu 1.
''Munaweza kuona nimetoa takwimu kubwa sana lakini tumeamua tuseme ukweli kwa sababu Watanzania sasa lazima waelewe kuwa tunakabiliwa na changamoto kubwa." alisema waziri huyo.

Ameongezea kwamba Idadi ya watu waliopona ni 11 huku waliofariki wakiwa 5.
Vilevile amewataka Watanzania kuchukua tahadhari kubwa kujilinda dhidi ya ugonjwa wa Corona.
"Kama kuna mmoja alikuwa na shauku basi ni wakati afahamu Corona inaanza na wewe kujikinga na pia uwakinge wengine"
Aidha afisa huyo wa serikali amesema kwamba kuna watu wenye dalili za ugonjwa wa corona ambao wamekuwa wakienda kupata huduma za matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kutokana na hilo ametoa wito kwa hospitali hiyo kutopokea wagonjwa kama hao akisema kwamba Muhimbili ni hospitali kuu ya rufaa inayokabiliana na magonjwa mengine na badala yake akawataka wagonjwa hao kuripoti katika hospitali ya rufaa ya mkoa ya Amana mjini Dar es Salaam.
Idadi hiyo ni kubwa zaidi kutangazwa kwa siku moja katika taifa la Afrika mashariki tangu wagonjwa wa kwanza wa virusi hivyo kugunduliwa katika eneo hili.

Waziri wa Afya nchini Tanzania Ummi MwalimuWatanzania watenga siku tatu za maombi

Hatua hiyo inajiri siku moja tu baada ya Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania kuwaomba raia wa taifa hilo kutenga siku tatu kuanzia tarehe 17 hadi 19 Aprili 2020, kumuomba Mwenyezi Mungu ili kuwaepusha na janga la ugonjwa wa corona.

Mikutano ya ibada inaruhusiwa nchini Tanzania.
Katika chapisho lake la mtandao wa Twitter Magufuli aliwataka raia wa taifa hilo kusali na kwa imani yake Mungu atawasikia.

Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 {Ijumaa, Jumamosi na Jumapili} KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia.

Wazanzibari waonywa dhidi ya kujitibu

Kulingana na taarifa hiyo wagonjwa hao ni kati ya umri wa miaka 20 hadi 66 na hawana historia yoyote ya kusafiri nje ya nchi katika siku za hivi karibuni.
Waziri huyo wa Afya amewasisitizia wananchi ambao wana dalili za homa kali, kukohowa na kupiga chafya kujitokeza katika vituo vya Afya au kupiga simu nambari 190.
'' Ni vyema mgonjwa mwenye dalili za maradhi haya asijichanganye na wagonjwa au watu wengine na tuache tabia ya kujitibu wenyewe kwani kwa kufanya hivyo tutendelea kueneza maambukizi na vifo vinavyohusiana na ugonjwa huo'', alisema bwana Hamad Rashid katika taarifa yake.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post