Na Joachim Nyambo,Mbeya.
WAZAZI
mkoani Mbeya wametakiwa kutambua kuwa katika kipindi hiki cha Mapambano
dhidi ya Covid-19 ni muhimu kuchukua tahadhali ili kuwalinda watoto wao
wanaporejea majumbani wakitokea kwenye mizunguko ya utafutaji au maeneo
ya starehe.
Tahadhali
hiyo inatokana na mazoea yaliyojengeka kwa wanajamii wengi kuwa na
tabia ya kuwakumbatia watoto wao hususani wadogo wanaporejea majumbani
wakitokea kwenye mizunguko ya kila siku.
Mkuu
wa mkoa wa Mbeya,Albert Chalamila amesema kuwakumbatia watoto mara
baada ya kurejea nyumbani kwa sasa si ufahari bali kunahatarisha afya ya
watoto hao hususani walio wachanga kwakuwa wako katika makundi
yanayotajwa kuwa hatarini kwa miili yao kuwa na kinga zilizo chini.
Chalamila
aliyasema hayo alipozungumza na watu wanaofanya shughuli zao katika
kituo cha Mabasi cha Mbalizi wilayani Mbeya alikokwenda kutoa elimu
kwaajili ya kujikinga na na virusi vya Corona.
“Ndugu
zangu ile tabia ya kumkumbatia mwanao unaporudi nyumbani kuwa ndiyo
upendo kwa wakati huu hebu tuiache.Unatoka ulikotoka kama ni kazini au
ni Baa unakwenda moja kwa moja unakinyenyua kitoto kichanga na kujifanya
ndiyo unaonesha upendo unahatarisha maisha yake.”
“Acha
watoto wakuone kama umepunguza upendo lakini lengo ni kuwalinda.Muhimu
kwa sasa unapofika nyumbani zingatia kwanza kunawa mikono na pia nguo
ulizoshindanao huko hebu zivue kwanza ndipo ukutane na watoto.Huwezi jua
ulimopita umebeba maambukizi.”alisisitiza.
Chalamila
pia aliwasihi wazazi na walezi mkoani hapa kuwa makini na utoaji zawadi
kwa watoto wao wanaporejea majumbani kwakuwa vifuangashio navyo
vinaweza kuwa na maambukizi kutoka kwa mtu mmoja na baada ya kufungia
bidhaa vikawa vimetumika kupeleka virusi hivyo kwa watoto nyumbani.
Aliwakumbusha
pia kuwasimamia watoto majumbani kuwa na tabia ya kutoshirikiana vyombo
wanaponywea vinywaji kama alivyowataka pia watu wazima kuachana na
tabia ya kuchangia vyombo vya kunywea wawapo vilabuni kwakuwa kufanya
hivyo kuna hataraisha maisha yao.
Kwa
upande wao baadhi ya wakazi katika mji huo wa Mbalizi walikiri baadhi
yao kuendelea na tabia ya kuzurula na watoto wadogo kwenye maeneo yenye
watu wengi yakiwemo masoko jambo walilosema elimu zaidi inahitajika kwa
wazazi na walezi ili kuondokana na tabia hiyo.
Wakazi
hao pia waliwataka wataalamu wa afya kuendelea kutoa ushauri wa
kitaaluma kwa wazazi na walezi waliowazoesha watoto wao kuchezea simu
zao wanaporudi majumbani jambo walilosema huenda njia hiyo pia ikawa
hatari kwa kusambaza virusi.