|
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha Jonathan Shana akipokea barakoa 2000 kwa ajili ya Jeshi la Polisi mkoani Arusha zilizotolewa na Kampuni ya A to Z ya mkoani hapa ikiwa ni kuendeleza Juhudi za Serikali kwenye mapambano dhidi ya Ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha |
|
Viongozi wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wakifuatilia hafla ya kupokea vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 iliyofanyika kwenye Ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha leo jijini Arusha |
|
Sehemu ya washiriki kutoka Taasisi za Jeshi la Polisi Magereza Uhamiaji Usalama wa Taifa kwenye hafla ya makabidhiano ya Barakoa 10,000 zilizotolewa na Kampuni ya A to Z kwa Serikali mkoa wa Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha |
|
Kutoka kushoto ni Meneja wa kiwanda Cha A to Z Binesh Haria,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Joseph Massawe anayefuati ni Mkurugenzi Mtendaji mkuu wa Kiwanda Cha A to Z Shah Katikati ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo pembeni yake ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Zelothe Stephen wakiwa Meza kuu wakifuatilia Hafla hiyo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha |
|
Meneja wa Kiwanda Cha A to Z akitoa Taarifa ya Vifaa vya barakoa 10,000 ambavyo wameikabidhi Serikali ya mkoa wa Arusha ikiwa ni mapambano ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 |
|
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipokea vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 kutoka kwa Meneja Binesh na CEO wake Mr.Shah kwenye hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha leo Jijini hapa |
|
Makabidhiano ya vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 yakiendelea leo jijini Arusha kwenye Ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha |
|
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen akipokea vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa Kali ya mapafu Covid 19 kutoka kwa Meneja na CEO wa Kiwanda Cha A to Z leo jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha. |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
KIWANDA cha kutengeneza Nguo Cha A to Z cha jijini Arusha,kipo katika hatua za mwisho za kukamilisha utengenezaji wa vazi maalumu linalotumiwa na wataalamu wa afya maarufu PPE,litakalovaliwa wakati wa kuzikia watu watakaofariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona.
Hayo yameelezwa May 5 na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa AtoZ, Binesh Haria wakati akikabidhi msaada wa Barakoa 10,000,kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo.
Binesh, amesema kiwanda hicho tayari kimeshashona vazi hilo na limeshapelekwa ngazi husika za serikali ikiwemo Mamlaka ya udhibiti wa dawa TMDA kwa ajili ya kuhakikiwa na likipitishwa wataanza uzalishaji wake .
Kuhusu msaada walioutoa,Binesh,amesema kiwanda hicho kimeamua kutoa mchango wake wa vifaa kinga vya korona kama sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na ugonjwa wa Corona.
Akipokea msaada huo Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema mtu yoyote atakayekufa kwa Corona ndani ya Mkoa huo atazikwa kwenye makaburi yoyote yaliyopo katika Mkoa huo huku familia zikipewa Uhuru wa kushiriki maziko hayo kwa heshima zote kwa watu wasiopungua 10 .
Amesema wataalam wa afya watatakiwa kufuata taratibu zote za afya ikiwemo kujiridhisha watakavyoona inafaa na marehemu atasafirishwa ndani ya Mkoa wa Arusha baada ya tahadhari zote kuchukuliwa.
Amesema endapo mgonjwa amekufa kwa Corona au hajafa kwa korona watu kumi tu ndio watakaomzika marehemu lengo ni kupunguza mikusanyiko makaburini.
Awali Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shanna alimshukuru Rc Gambo kwa juhudi kubwa za kutafuta vifaa kwa ajili ya kujilinda na ugonjwa huo kutumia wadau na pia alishukuru kwa mgao wa barakoa 2000 walizopatiwa na kiwanda cha A TO Z.
Katika mgawanyo huo Uhamiaji walipewa barakoa 500,CCM Mkoa barakoa 1,000 na Jeshi la Magereza barakoa 1,500 huku barakoa nyingine zikigaiwa katika tarafa mbalimbali za Mkoa wa Arusha.