TIGO YAZINDUA KAMPENI YA "JAZA TUKUJAZE TENA" WATEJA KUZAWADIWA VIFURUSHI




Jumatatu, 25 Octoba 2020 – Kampuni ya mawasiliano inayoongoza kwa kutoa huduma za kidigitali nchini Tanzania, Tigo, leo imezindua kampeni ya siku tisini itakayofanyika nchi nzima ambayo imelenga kuwafanya wateja wote wa Tigo kuwa washindi wa zawadi mbalimbali kila wanaponunua bando za siku, wiki au mwezi.

Kampeni hii iliyopewa jina la ‘Jaza Tukujaze Tena’ inalenga kuwazadia wateja kutokana

na uaminifu wao kwa kampuni ya Tigo, hivyo ndani ya kipindi cha kampeni, wateja

wataweza kuzawadiwa dakika za muda wa maongezi, SMS, pamoja na MBs/GBs kila

watakoponunua bando.

Pia, mbali na wateja kuzawadiwa muda wa maongezi pamoja na MBs za bure,

kutakuwa na simu janja zaidi ya 1,200 ambazo pia watazawadiwa wateja. Simu janja

zitakazoshindaniwa ni pamoja na Samsung Note 20, ITEL T20 pamoja na Smart

Kitochi. Simu janja hizi zitashindaniwa na wateja wote wa Tigo, mawakala, viongozi wa

timu za mauzo na wahudumu wakubwa wa Tigo Pesa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Kaimu Afisa Mkuu Kitengo cha Biashara wa Tigo Tanzania, David Umoh, amesema, “Siku zote tumekuwa tukitafuta

njia mpya za kuwazawadia wateja wetu pamoja na wabia wetu, na tunapoingia miezi

miwili ya mwisho wa mwaka 2020, tunaamini kampeni hii itaweza kupamba sikukuu za

mwisho wa mwaka. Lengo la kampeni hii ni kuhakikisha kila mteja wa Tigo anakuwa

mshindi. Jaza Tukujaze Tena ni kampeni mahususi kwa ajili ya kutambua uaminifu wa

wateja pamoja na wabia wetu kama kampuni”.



Pia amesisitiza juu ya namna Tigo ilivyojidhatiti kuhakikisha inaendelea kubuni bidhaa

na huduma mpya zinazoendana na mabadiliko ya ulimwengu. “Ni muhimu sana kwetu

tunapokuja na kampeni inayogusa maisha ya wateja wetu moja kwa moja kwa sababu

wamekuwa wakitumia bidhaa zetu kila kukicha. Tigo imedhamiria kutengeneza msingi

wa wateja waaminifu kwa kampuni, na kupitia kampeni hii tunalenga kufanikisha hilo,”

amesema Umoh

“Tunaamini kwamba wateja wetu watafurahia kupata muda wa ziada wa dakika za

kupiga simu, SMS pamoja na data ambazo tutakuwa tunawazadia ili kurahisisha

maisha yao ya kila siku”, ameongeza Umoh.

Kwa wateja wetu kuzawadiwa ofa hizi za bure, wanapaswa kununua bando za siku, wiki

au mwezi kupitia menu yetu ya *147*00#, Tigo Pesa App pamoja na tovuti ya Tigo.

Wateja wote hawa wataweza kuingizwa moja kwa moja kwenye droo ambayo sasa

itawezesha washindi wa simu janja kupatikana.

Wasambazaji wa huduma mbalimbali za Tigo pia wataweza kuingizwa moja kwa moja

kwenye droo hii ili kuwa na nafasi ya kujishindia zawadi kemkem kila watakapouza

bando za aina yoyote kupitia Tigo Rusha.

Tigo Tanzania inapenda kuwataadharisha wateja wake wote kwamba wawe makini na

matapeli wanaoweza kuibuka kupitia mgongo wa kampeni hii. Wateja wanapaswa

kufahamu kwamba, zawadi zote za bando zitakuwa zinatolewa papo hapo mara tu

baada ya mteja kununua bando. Pia washindi wa simu janja wa kila siku pamoja na wiki

watapigiwa simu na mfanyakazi wa Tigo kupitia namba maalumu ya kampuni mara tu

baada ya droo hizo kufanyika. Ofa hii ni bure, washindi hawapaswi kutoa malipo ya aina

yoyote ili kupata zawadi zao.

Wateja wote wa Tigo wanashiriki katika ofa hii.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post