Uchumi wa Afrika kuporomoka kutokana na covid-19

 “Uchumi wa Afrika unaweza kupoteza kati ya dola bilioni 90 na 200 mwaka 2020”

Na Mwandishi Wetu, Arusha

TANGU kulipolipuka kwa ugonjwa wa mapafu maarufu kama corona (COVID -19), huko katika mji wa Huan katika jamhuri ya watu wa China na baadae kusambaa katika nchi zingine duniani, idadi kubwa ya watu wameshafariki na wengine wameendelea kufariki kila uchao kutokana na madhara ya ugonjwa huo.

Licha ya maafa yanayoendelea kutokea tiba ya Corona bado haijaweza kupatikana ijapokuwa matumaini yameanza kuonekana katika chanjo kadhaa ambazo zimeweza kugunduliwa na Mataifa mbalimbali duniani ikiwemo iliyogunduliwa hivi karibuni na wataalamu katika nchi ya Uingereza.

Nchi hiyo baada ya kugundua chanjo hiyo na kuifanyia utafiti wa kina, jumanne wiki hii Disemba 8, 2020 ilianza kuwapatia wananchi wake na baadae utaandaliwa utaratibu wa kuweza kuisambaza katika nchi zingine duniani.

Wakati wataalam wakiendelea na upatikanaji wa suluhu ya uhakika ya kutibia ugonjwa wa Corona, uchumi wa nchi nyingi barani Afrika unaelezwa kuendelea kuporomoka kwa kasi kutokana na sababu mbalimbali ambazo zinaelezwa kusababishwa na ugonjwa wa Corona.

Nchini Tanzania, licha ya ugonjwa wa Corona kutokuwepo kama mamlaka za Kiserikali zinavyoeleza, madhara yake ni makubwa kwa mustakabali wa uchumi wa nchi lakini pia kwa mwananchi mmoja mmoja.

Uchunguzi unaonyesha kuwa ugonjwa wa corona umesababisha kampuni nyingi kufunga uzalishaji na zingine kulazimika kupunguza wafanyakazi na hivyo tatizo la ukosefu wa ajira ambalo limekuwa likisumbua vichwa vya watawala wetu kwa namna ya kukabiliana nalo kuendelea kuongezeka kwa kasi kubwa.

Mbali ya Tanzania, bara zima la Afrika limekumbwa na sintofahamu ya namna ya kukabiliana na matokeo ya ugonjwa wa Corona katika nyanja ya kiuchumi kufuatia kupungua kwa uzalishaji kwa asilimia kubwa.

Sekta ya viwanda ambayo ndio kiungo cha kutoa ajira imeendelea kudidimia katika nchi nyingi barani humo na kuhatarisha uchumi wa Serikali lakini pia uchumi wa mtu mmoja mmoja katika kujipatia mahitaji yake ya msingi.

Katika utafiti uliofanywa hivi karibuni, uchumi wa Afrika unaelezwa kuweza kupoteza kati ya dola za kimarekani Bilioni 90 hadi bilioni 200 kwa mwaka 2020 kutokana na madhara ya ugonjwa wa Corona kulingana na utafiti uliopewa jina la Tackling COVID-19 barani Afrika, ambao ulitolewa wiki hii na wataalam wa kampuni ya Kimataifa ya ukaguzi ya McKinsey & Company.

Imegunduliwa kuwa hasara hizi zimetokana na kupungua kwa matumizi ya kibinafsi na marufuku ya kusafiri kuenea barani Afrika, na vile vile kuahirishwa kwa uwekezaji kutoka mataifa ya nje.

Wakati athari za uchumi zikiendelea huku bei ya mafuta ikishangaza wengi barani Afrika kwa kuendelea kupana kila uchao,hali hii ya kiuchumi itajidhihirisha kwa njia tofauti katika mataifa mengine kama vile Nigeria, Afrika Kusini, Kenya na Tanzania.

Ripoti hiyo imeshauri Serikali za Kiafrika na washirika wa maendeleo ikiwemo mashirika ya kimataifa kufanya utafiti wa njia mbadala za kupata suluhisho kama vile kuwa na mipango ya maendeleo ya kiuchumi.


Aidha ripoti hiyo ilipendekeza pia "Mfuko wa Ushirikiano wa Afrika" ambao unaruhusu wafanyabiashara na watu kuchangia juhudi za misaada kwa "biashara zilizo hatarini zaidi." Ili kunusuru uchumi katika nchi hizo.

Zaidi ya hayo, mfuko wa sekta binafsi unaweza kuanzishwa kwaajili ya kutoa misaada, mikopo ili "kusaidia biashara na kupunguza upotezaji wa kazi." Jambo ambalo linahitaji tafakuri na busara ya hali ya juu.

 

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post