WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA ELIMU KUJIKINGA NA WANYAMAPORI

 

Afisa wanyamapori mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Antonia Raphael akitoa ufafanuzi kwa wanawake kuhusu utaratibu wa malipo ya kifuta machozi kwa wakazi wa kijiji cha mheza wilayani same, mkoani Kilimanjaro.

Washiriki wa mafunzo wakichanganya pilipili na mchanga ili kutengeneza vilipuzi salama kwa kufukuza Tembo Shambani kwenye mafunzo ya mbinu za kudhibiti migongano baina ya wanyamapori wakali na waharibifu katika kijiji cha Muheza wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Washiriki wa mafunzo wakiwa kwenye mafunzo ya ujenzi wa uzio wa kudhibiti Tembo kuingia Shambani na kuharibu mazao kwenye mafunzo ya mbinu za kudhibiti migongano baina ya wanyamapori wakali na waharibifu kwenye kijiji cha Muheza ,wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro

Washiriki wa mafunzo wakipatiwa elimu ya uwekaji wa mizinga ya nyuki kando ya shamba kwa ajili ya kulinda mazao dhidi ya Tembo kwenye mafunzo ya mbinu za kudhibiti migongano baina ya wanyamapori wakali na waharibifu aliyofanyika kwenye Kijiji cha Muheza, wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.


Wizara ya Maliasili na Utalii imewataka wananchi wa Kata ya Maore wilayani Same mkoani Kilimanjaro kutumia kwa usahihi mafunzo ya kujikinga na wanyamapori ili waweze kuyalinda mazao yao bila ya kusababisha madhara kwa wanyamapori.

Akizungumza na wananchi Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) Dkt. Emmanuel Masenga amesema endapo wananchi watayatumia vema mafunzo hayo watapunguza kwa kiasi kikubwa ugumu wa kazi ya kufukuza Tembo mashambani. Aidha, Dkt. Masenga amewakumbusha wananchi kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo kwenye maeneo ya jirani na hifadhi.

Kwa upande wake, afisa wanyamapori mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii , Bi. Antonia Raphael amesema mafunzo hayo yatakuwa endelevu katika maeneo mengine lakini pia wizara imeweka Utaratibu mzuri wa ufuatiliaji wa wale wote waliopata mafunzo hayo ili kuona kama wanatekeleza kile walichojifunza.

Mafunzo hayo kwa vitendo yalihitimishwa leo kwa wananchi wa Same na baadae washiriki waliofuzu walipatiwa vyeti.

This is received, thanks for your comments, will come back to you

Previous Post Next Post